Shirika la maendeleo la Ufaransa AFD lashirikiana na serikali ya Kenya kubadilisha maisha ya raia
Nairobi – Shirika la maendeleo la Ufaransa AFD kwa ushirikiano na serikali ya Kenya imefanya miradi kadhaa iliyogharimu takribani Euro milioni 135 ili kuimarisha maisha ya wakenya wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda jijini Nairobi na hata katika miji mingine kama Kisumu .
Imechapishwa: Imehaririwa:
Cheza - 01:54
Shirika hilo la ufaransa limewekeza mamilioni ya fedha ili kujenga barabara,kuweka mifereji ya maji , kuunda mitaro ya kupitisha maji chafu na kuweka taa za barabarani katika juhudi za kuimarisha maisha ya wakenya katika maeneo tofauti tofauti kama vile Kayole Soweto.
RFI imefanikiwa kuzungumza na Mkurugenzi wa shirika hilo kwenye ukanda wa Afrika, Helene Ngernim-Ganga ili kueleza zaidi kuhusu shirika lao AFD na nini malenge yao
Kwa sasa tunafanya kazi na tuna miradi mingi ya maendeleo ,miundombinu ,nishati ,miradi ya utoaji maji safi na usafi wa mazingiria kwa jumla.Pia tumewekeza kwa kiasi cha Zaidi ya asilimia 50 na tunazidi kukua katika sekta za kijamii kama vile elimu na afya.Alisema Helene Ngernim-Ganga
HELENE GANGA DIRECTOR AFD
Katika mtaa huo wa Kayole Soweto nilizungumza na Jane Wangare ambaye amefaidika pakubwa na mradi huo wa barabara na taa
JANA WANGARE MKAAZI SOWETO
Vilevile Hezron Ongesa anayesimamia kundi la vijana katika eneo hilo amelisifu shirika hilo kwa kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 200
HEZRON ONGESA MKAAZI SOWETO
Kufikia sasa AFD imewekeza euro milioni 35 huku benki kuu ya dunia ikitoa euro milioni 100 ili kufanikisha miradi hiyo.