Pata taarifa kuu

Wataalam wa afya na safari za angaa wakutana Mombasa kujadili hali ya Uviko 19

NAIROBI – Watalaam kutoka sekta ya usafiri wa anga kutoka mataifa 15 barani Afrika wanakutana mjini Mombasa pwani ya Kenya kujadili na kutathmini hatua ambazo zilichukuliwa wakati wa kudhibiti milipuko ya virusi vya Uviko -19, Ebola na Marburg barani Afrika.

Sehemu kubwa ya mataifa ya dunia yameondoa vikwazo vya kudhibiti maambukizi ya uviko 19
Sehemu kubwa ya mataifa ya dunia yameondoa vikwazo vya kudhibiti maambukizi ya uviko 19 AFP - PAU BARRENA
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya maswala yanayojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na namna mataifa mbalimbali barani Afrika yameweka mikakati ya kuzuia magonjwa ya kuambukiza kuingia nchini mwao kupitia abiria wanaotoka mataifa za kigeni wanaosafiri kwa ndege na uwepo wa teknolojia za kisasa zinazochunguza na kubaini iwapo abiria hajaambukizwa magonjwa hayo.

Tayari taifa la Kenya limeondoka kutoka kwa mbinu ya tiba dhidi ya uviko -19 hadi uzuiaji wa maambukizi ya virusi hivyo kwa kukumbatia huduma za wahudumu wa afya nyajani, ambao wanauguza na kuwatunza wagonjwa wanaoishi na ulemavu na wakongwe nyumbani kama njia mojawapo ya kupunguza idadi ya wagojwa hospitalini.

Mary Muthoni ni katibu mkuu katika wizara ya afya.

“Hatutaki kungoja mpaka mtu anapokabiliwa na ugonjwa ndio aende kumuona dakatari tungependa kuwa na uwezo wa kuzuia magonjwa yote.” alisemaMary Muthoni ni katibu mkuu katika wizara ya afya

00:09

Mary Muthoni ni katibu mkuu katika wizara ya afya

Iyubuntu Jilson - Afisa kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Burundi amesema wameweka mifumo ya uchunguzi wa kimatibabu kwa wasafiri katika viwanja vya ndege.

Kwenye uwanja wa ndege walijenga kituo cha uchunguzi pamoja na mikakati ambayo ilikuwa inasaidia wasafiri kuomba nafasi ya kuhudumiwa kabla ya kutua”alielezaIyubuntu Jilson.

00:07

Iyubuntu Jilson kutoka Burundi

Taifa la Tanzania pia limewakilishwa na Daniel Malanga – afisa kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga….

Tumekuja kupata uzoefu wa namna ya kukabiliana na maambukizi labda ya uviko 19, Ebola na Marburg tumekuja kujifunza hapa kupitia wenzetu walio na huo uzoefu.” alisemaDaniel Malanga – afisa kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga kutoka Tanzania.

00:11

Daniel Malanga kutoka Tanzania

Shirika la afya duniani – WHO, imezitaka nchi za Afrika kuimarisha sekta za afya katika viwanja vya ndege ili kuzuia magonjwa ya kuambukiza ambayo yanaweza kuambukizwa kutoka nchi hadi nchi kupitia usafiri wa anga.

Diana Wanyonyi, Mombasa - RFI Kiswahili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.