Pata taarifa kuu

Kabuga, hayupo katika hali nzuri ya kiafya ili kushtakiwa: Mahakama

NAIROBI – Majaji katika mahakama ya umoja wa mataifa kuhusu uhalifu wa kivita wameamua kwamba mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini  Rwanda Félicien Kabuga, hayupo katika hali nzuri ya kiafya ili kushtakiwa. 

Félicien Kabuga (picha ya kumbukumbu).
Félicien Kabuga (picha ya kumbukumbu). Nations Unies/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kabuga, mwenye umri wa miaka 90, ni tajiri wa zamani anashtumiwa kuanzisha kituo cha utangazaji cha chuki ambacho kilichochea mauaji ya ya karibu watu 800,000 wengi wao Watusti. 

Kesi ya Kabuga ilianza kusikilizwa katika mahakama ya The Hague mwezi Septemba mwaka uliopita.  

Majaji wamesema wataalam wa afya  wamegundua kuwa alikuwa na changamoto za kiakili na hakuweza kushiriki ipasavyo mahakamani.  

Aidha, majaji hao sasa wanapendekeza njia mbadala ya kuendelea na kesi dhidi ya Kabuga, nje ya Mahakama ili haki itendeke. 

Kabla ya kufanyika kwa uchunguzi huo, Mfanyabiashara huyo alikataa kufika Mahakamani na baadaye kufuatilia kwa njia ya video akiwa katika eneo anakozuiwa. 

Kabuga, alikamatwa jijini Paris mwaka 2020 baada ya kukwepa mkon wa sheria kwa miaka 26. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.