Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya majenerali wawili wanaopigana nchini Sudan
NAIROBI – Marekani, imeziwekea vikwazo kampuni zinazohusishwa majenerali wawili wanaopigana nchini Sudan, katika mkakati wa kumaliza vita hivyo jijini Khartoum na nje.
Imechapishwa:
Wizara ya fedha Marekani ,imesema imelenga kampuni kubwa mbili zinazohusishwa na jeshi na pia wapiganaji wa kikosi cha RSF na ambazo zinatuhumiwa kuchangia mapigano hayo nchini Sudan.
Kampuni hizo ni pamoja na Al Junaid Multi Activities Co Ltd na Tradive General Trading, zinazohushwa na RSF na Defense Industries System na Sudan Master Technology, zinazohushwa na jeshi la Sudan.
Waziri wa fedha wa Marekani ,Janet Yellen amesema lengo kubwa ni kukata ufadhili unaochochea vita hivyo.
Hatua hii inajiri baada ya pande zote kushindwa kuheshimu makubaliano ya kusitisha vita na kuruhusu usambazaji wa msaada.
Alhamis ya wiki hii ,watu 18 waliwauwa na wengine 100 kujeruhiwa ,katika shambulio la roketi kwenye soko moja jijini Khartoum.