Pata taarifa kuu

AU kuendelea na upatanisho nchini Sudan

NAIROBI – Umoja wa Afrika umesema hatua ya kusitishwa kwa mazungumzo kati ya pande zinazohasimiana nchini Sudan, haifai kuchukuliwa kama kuachana na juhudi za kuleta upatanisho nchini humo na kumaliza vita.

Jeshi la Sudan limesema limesitisha mazungumzo na kundi la RSF
Jeshi la Sudan limesema limesitisha mazungumzo na kundi la RSF © Forces armées soudanaises / via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya AU inakuja baada ya siku ya Jumatano ,uongozi wa jeshi la Sudan ,kusitisha mazungumzo na kikosi maalum cha RSF, vyanzo kutoka jeshi vikisema hatua hiyo ilisababishwa na RSF kutoheshimu  makataa ya amri ya usitishwaji wa vita ,likiwemo kuwaondoa wapiganaji wake kwenye hospitali na maeneo wanaokaa raia.

Hata hivyo umoja wa Afrika, umesema mabadiliko hayo hayastahili kulemaza juhudi za kutafuta mwafaka wala kuwavunja moyo wapatanishi ambao ni Marekani na Saudi Arabia ambao wamefanya kazi kubwa.

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na wapiganaji wa RSF yamesababisha vifo vya raia na uharibifu wa mali
Mapigano kati ya jeshi la Sudan na wapiganaji wa RSF yamesababisha vifo vya raia na uharibifu wa mali AFP - -

Mkuu wa wafanyikazi katika ofisi ya rais ya Umoja huo Mohammed El Hacen Lenatta amesema, katika mazungumzo magumu kama hayo, misimamo kama hiyo inatarajiwa kutokea.

Mazungumzo hayo yamekuwa yakiendelea tangu mapema Mei na yamechangia kuwepo kwa makubaliano mawili ya kusitishwa vita ambayo hata hivyo yamekiukwa.

Mapigano mapya yalishuhudiwa jumanne siku ambayo majenerali wawili walikuwa wamekubaliana kuongeza muda wa kutekeleza makubaliano ya kusitisha vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.