Pata taarifa kuu

Sudan: Wapatanishi wanataka muda wa usitishaji mapigano kuongezwa

NAIROBI – Marekani na Saudi Arabia, zinazoongoza jitihada za kupatanisha pande mbili zinazopigana nchini Sudan, zinataka muda wa kusitisha mapigano uongozwe.

Makundi mawili ya kijeshi yamekuwa yakipigana nchini Sudan, raia wakionekana kuathirika
Makundi mawili ya kijeshi yamekuwa yakipigana nchini Sudan, raia wakionekana kuathirika AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa ya pamoja, wasuluhishi kutoka mataifa hayo mawili wanataka jeshi na wanamgambo kuongeza muda huo unaokamilika saa tatu na dakika 45, usiku ili kuendelea kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia raia wa kawaida.

Aidha, pande hizo mbili zimetakiwa kuendelea kuzungumza ili kufikia mwafaka huo kwa manufaa ya raia wa Sudan ambao kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa wameshuhudia vita ambavyo vimesababisha zaidi ya watu elfu 1 kupoteza maisha.

Wakati wito huo ukitolewa, kuliripotiwa makabiliano ya risasi kati ya pande hizo mbili jijiini Khartoum hapo jana Jumapili, huku kila upande ukimlaumu mwenzake.

Kwa kipindi cha wiki moja cha usitishwaji wa vita, kumeshuhudiwa mkataba huo ukivunjwa mara kadhaa jijini Khartoum, lakini kwa kiasi kikubwa, utulivu umekuwa ukishudiwa, kinyume na hali ilivyokuwa hapo awali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.