Pata taarifa kuu
ULINZI-DIPLOMASIA

Felix Tshisekedi kwa mara nyingine anahoji kuhusu kikosi cha EAC kilichotumwa DRC

Kando ya ziara yake ya kiserikali nchini China, Rais wa DRC kwa mara nyingine amekosoa kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kilichotumwa mashariki mwa nchi yake kupigana hasa dhidi ya waasi wa M23. Félix Tshisekedi, kwa upande mwingine, hkuzungumzia kikosi cha Burundi, wakati wa mkutano na raia wa DRC waishio China.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi akihudhuria mazungumzo na Waziri Mkuu wa China Li Qiang kwenye Ukumbi wa Great Hall of the People mjini Beijing, China Mei 26, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi akihudhuria mazungumzo na Waziri Mkuu wa China Li Qiang kwenye Ukumbi wa Great Hall of the People mjini Beijing, China Mei 26, 2023. REUTERS - THOMAS PETER
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Kongo anaendelea na ziara yake rasmi nchini China. Ijumaa hii, Mei 26, amekutana na mwenzake Xi Jinping mjini Beijing. Sasa anatarajiwa kwenda Shenzhen, Shanghai na Hong Kong.

Alipowasili China, Felix Tshisekedi alikwenda kukutana na raia wa DRC waishio China ambapo alizungumza kwa kirefu mbele yao. Amewahakikishia kwamba uchaguzi wa urais utafanyika Disemba 20, na kukashifu msimamo wa upinzani, ambao "haujui unachotaka". "Ameshutumu mambo kadhaa, ameshutumu Tume Huru ya Uchaguzi (CENI), Mahakama ya Katiba. Hatimaye, wapinzani hawa hata hivyo walijiunga na mchakato wa uchaguzi,” ameongeza.

Mkuu wa Nchi pia amerejelea hali ilivyo mashariki mwa DRC, akishutumu "uchokozi wa kikatili na wa kinyama kwa upande wa Rwanda", akimaanisha mzozo na M23. Kinshasa imeishutumu Rwanda kwa miezi kadhaa kwa kuwasaidia waasi wa M23 walioteka sehemu ya mkoa wa Kivu Kaskazini kabla ya kurudisha ngome zake kwa wanajeshi wa Jeshi la Afrika Mashariki (EAC). Shutuma zilizorejelewa na Umoja wa Mataifa na babalozi wa nchi kadhaa za Magharibi, lakini zifutiliwa mbali kabisa na Kigali.

Kikosi cha Burundi hakijakosolewa

Rais pia kwa mara nyingine amehoji hatua ya EAC inayojumuisha wanajeshi kutoka Burundi, Sudan Kusini, Uganda na Kenya. Lawama hizo zimewalenga zaidi wanajeshi wa Kenya na Uganda, wanaoshutumiwa na rais kwa "aina ya ushirikiano kati ya kikosi cha EAC na waasi au magaidi wa M23". Na kuongeza: “isipokuwa kikosi cha Burundi ambacho kinatumika katika maana halisi ya neno, makubaliano kama yalivyopangwa. Kama uthibitisho wa hili, uingiliaji kati wa Warundi wakati magaidi wa M23 walipoanza kutoza ushuru kinyume cha sheria katika maeneo waliyoyamiliki. Kwa majeshi mengine kutoka jumuiya hiyo, wanaendelea kuishi pamoja na magaidi wa M23, " amebaini.

Kwa miezi kadhaa, Kinshasa imekuwa ikikosoa kikosi hiki cha kikanda, hasa kwa kutotumia mamlaka inayoelezwa na mamlaka ya DRC kuwa "mashambulizi" dhidi ya waasi. Hata hivyo rais Tshisekedi alibaini kwa uwazi, takriban siku kumi zilizopita, akizuru Botswana, kwamba siku za misheni hiyo zinahesabika: mamlaka inapaswa kumalizika mwishoni mwa mwezi Juni.

Hivi karibuni majeshi kutoka kusini mwa Afrika, SADC yatapelekwa DRC na yatachukuwa nafasi ya kikosi cha jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC. Wanaweza kuanza kutumika kati ya Juni 15 na 20, kulingana na Kinshasa. Mkutano wa wakuu wa majeshi utafanyika katika siku zijazo ili kuweka masharti.

Wakati huo huo, Waziri wa Ulinzi wa Malawi, Harry Mkandawire, alisafiri hadi Goma mapema wiki hii ili kuhakikisha nchi yake inashiriki katika kurejesha amani mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.