Pata taarifa kuu

Sudan: Mamia ya raia wasubiri kuwasili kwa misaada ya kibindamu

NAIROBI – Mamia ya raia kwenye mji mkuu wa Sudan, Khartoum pamoja na miji jirani, wanaendelea kusubiri kwa hamu kufika kwa misaada ya kibinadamu, siku chache tangu kuanza kutekelezwa kwa mkataba wa usitishaji mapigano kati ya pande zinazohasimiana.

Watoto wakimbizi wa Sudan ambao wamekimbia ghasia katika eneo la Darfur karibu na mpaka wa Sudan na Chad huko Koufroun, Chad.
Watoto wakimbizi wa Sudan ambao wamekimbia ghasia katika eneo la Darfur karibu na mpaka wa Sudan na Chad huko Koufroun, Chad. © REUTERS - ZOHRA BENSEMRA
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa hali ya utulivu imeshuhudiwa katika maeneo mengi ya nchi licha ya kuwa hapo jana kuliripotiwa mashambulio kadhaa ya anga kwenye mji wa Khartoum, ingawa nchi za Marekani na Saudi Arabia ambazo ndio wasimamizi wa mkataba huo wanasema hali ni tofauti na siku chache zilizopita.

Hata hivyo licha ya kuripotiwa kwa hali ya utulivu na makabiliano kidogo, wasimamizi wa mkataba huo wamezituhumu pande zote mbili kwa kukiuka sehemu ya makubaliano hayo, ambapo wameonya kuchukua hatua.

Aidha umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya misaada ya kibinadamu, imesema tayari pande hasimu zimetenganishwa na kwamba ndani ya saa chache zijazo baadhi ya misaada itaanza kuwafikia raia waliokuwa wamenasa katika mapigano.

Haya yanajiri wakati huu mkuu wa majeshi ya Sudan jenerali Abdel Fattah al Burhani na mwenzake Mohamed Dagalo, wakiahidi kuheshimu makubaliano hayo, licha ya kwamba kila mmoja anaamini ataibuka mshindi katika vita yao ya kuwania madaraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.