Pata taarifa kuu

Mkuu wa redio inachosikilizwa zaidi nchini Tunisia kuachilia huru

Mahakama ya Tunisia imeamua siku ya Jumatano kumwachilia huru mkuu wa Mosaïque FM, redio inachosikilizwa zaidi nchini Tunisia, baada ya takriban miezi minne ya kuzuiliwa kwa utakatishaji fedha na "njama dhidi ya usalama wa serikali", shirika la habari la AFP limepata taarifa hii kupitia wakili wake.

Waandishi wa habari wa Tunisia walikusanyika mjini Tunis kwa ajili ya maandamano ya uhuru wa vyombo vya habari mnamo Februari 16, 2023, siku nne baada ya kukamatwa kwa Noureddine Boutar, mkurugenzi mkuu wa redio Mosaïque FM.
Waandishi wa habari wa Tunisia walikusanyika mjini Tunis kwa ajili ya maandamano ya uhuru wa vyombo vya habari mnamo Februari 16, 2023, siku nne baada ya kukamatwa kwa Noureddine Boutar, mkurugenzi mkuu wa redio Mosaïque FM. AP - Hassene Dridi
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Rufaa ya kitengo cha fedha cha Tunis imekubali ombi kutoka kwa upande wa utetezi kumwachilia Noureddine Boutar, lakini kwa sharti la malipo ya dhamana ya dinari milioni moja (sawa na euro elfu 300), amebaini wakili Dalila Msaddek. Haruhusiwi kuondoka kwenye ardhi ya Tunisia, ameongeza.

“Bw. Boutar hana kiasi hiki hasa kwa vile mahakama imemzuilia mali zake zote, tupo kwenye mchakato wa kukusanya kiasi hiki, hivyo itakuwa vigumu kwake kuachiwa leo,” amesema Msaddek. Alikamatwa Februari 13 wakati huo huo na wapinzani na viongozi wengine, wanaoshukiwa kupanga njama dhidi ya taifa la Tunisia, na ambao Rais Kais Saied aliwataja kuwa ni "magaidi".

Jaji alitoa hati ya kukamatwa dhidi ya Bw. Boutar kwa madai ya ufujaji wa pesa, kesi ambayo anaendelea kufunguliwa mashitaka, kama vile faili linalomshtaki kwa njama. Daima amekuwa akipinga kutokuwa na hatia yoyote, akidai kuwa amekamatwa kwa sababu ya redio yake, ambayo inatoa nafasi kubwa kwa raia kutoa maoni yao.

Wanahabari wengine wa Mosaïque FM pia wamefunguliwa mashtaka. Waandishi wawili nyota wa redio hii, Haythem El Mekki na Elyes Gharbi, walikaguliwa mapema wiki hii na kikosi cha polisi kwa kutaja katika kipindi chao kinachopendwa cha "Midi Show" mapungufu katika kuajiri maafisa wapya katika idara za usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.