Pata taarifa kuu

Senegal:Watatu wafariki baada ya mzozo kati ya polisi na wafuasi wa kiongozi wa upinzani

Nairobi – Watu watatu wamefariki  baada ya mzozo kati ya polisi na wafuasi wa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko aliefikishwa mahakamani kwa shtuma za ubakaji.Kukamatwa kwa Sonko hapo Machi mwaka 2021 kulisababisha siku kadhaa za ghasia mbaya ambapo watu wasiopungua 12 waliuawa.

Picha iliyopigwa Machi 2021. Mpinzani wa kisiasa Ousmane Sonko alishinda ukumbi wa jiji la Ziguinchor katika uchaguzi wa mitaa mnamo Januari 23, 2022.
Picha iliyopigwa Machi 2021. Mpinzani wa kisiasa Ousmane Sonko alishinda ukumbi wa jiji la Ziguinchor katika uchaguzi wa mitaa mnamo Januari 23, 2022. AP - Sylvain Cherkaoui
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya mambo ya ndani mapema leo imesema kuwa imejulishwa kuhusu vifo vya vya watu tatu.Mmoja anasemekana aliuwawa kwa kuchomwa kisu katika jiji la Dakar  wakati yule wa pili alipatikana Ziguinchor.Hata hivyo wizara hiyo imetoa wito kwa wazazi kulinda watoto wao kujihusisha na vurugu hizo.

Matukio haya yanahusishwa na mashambulizi, wizi, uporaji na vitendo vingine vya uharibifu.

Siku ya Jumatatu, wizara hiyo ilisema kuwa polisi alikufa baada ya kukanyagwa na gari la kivita ambalo lilikuwa limetumwa kwenye maandamano huko Ziguinchor.

Umati wa watu ulifunga barabara kwa magogo na matairi yaliyochomwa , wakiwarushia mawe polisi ambao walijibu kwa mabomu ya vitoa machozi, kwa mujibu wa mwandishi wa AFP.

Vyombo vya habari vya ndani viliripoti kuwa waandamanaji kadhaa wamejeruhiwa.

Maandamano huko Ziguinchor na eneo la Dakar yalizuka usiku wa kuamkia leo ambapo Sonko alikua anafikishwa mahakamani. Sonko anakabiliwa na kesi ya ubakaji wa mfanyakazi katika saluni ambapo alienda kukandwa misuli.

Kesi hiyo ilifunguliwa akiwa hayupo katika mahakama ya Dakar siku ya Jumanne na kuahirishwa mara moja hadi Mei 23.

Sonko, mwenye umri wa miaka 48, ambaye pia hivi majuzi alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kumkashifu na kumtusi waziri wa utalii, amekana shtaka hilo.

Sonko, rais wa chama cha Pastef-Patriots, alishika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa urais wa 2019.

Anasema kesi za kisheria dhidi yake ni njama inayolenga kumzuia kuwania kura ya 2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.