Pata taarifa kuu

Chama cha upinzani cha Tunisia kimeshutumu vikali hukumu ya kisiasa dhidi ya Ghannouchi

Nairobi – Chama cha Ennahdha chenye mfungamano na  wa Waislam wa Tunisia siku ya Jumanne kimelaani hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja jela iliyotolewa kwa kiongozi wake Rached Ghannouchi, na kuiita "hukumu isiyo ya haki ya kisiasa".

Kiongozi wa Chama Cha Kiislam Cha Tunisia Rached Ghannouchi akiwa kwenye moja ya kampeni
Kiongozi wa Chama Cha Kiislam Cha Tunisia Rached Ghannouchi akiwa kwenye moja ya kampeni REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Ghannouchi, mpinzani mkuu wa Rais Kais Saied, alihukumiwa Jumatatu kwa mashtaka yanayohusiana na ugaidi kufuatia kukamatwa kwake Aprili 17.

Alikuwa amefikishwa mahakamani mwishoni mwa Februari kujibu mashtaka baada ya kushtakiwa kwa kuwaita maafisa wa polisi "wadhalimu".

Kesi hiyo ilikuwa mojawapo ya kesi zilizotozwa na mamlaka dhidi ya Ghannouchi, ambaye chama chake kilikuwa kikubwa zaidi bungeni kabla ya Saied kuvunja bunge mnamo Julai 2021 kama sehemu ya kunyakua mamlaka iliyomruhusu kutawala kwa amri.

Kabla ya kuzuiliwa kwake, spika huyo wa zamani wa bunge mwenye umri wa miaka 81 alisema kuwa kutokomeza mitazamo tofauti, kama vile Uislamu wa kushoto au wa kisiasa, kunaweza kusababisha "vita vya wenyewe kwa wenyewe".

"Tunalaani hukumu iliyotolewa dhidi ya Rached Ghannouchi, ambayo tunaiona kama uamuzi usio wa haki wa kisiasa, na tunaomba aachiliwe," Ennahdha ilisema katika taarifa yake.

Mbali na kifungo cha mwaka mmoja jela, Ghannouchi alitozwa faini ya dinari 1,000 (dola 326).

Ghannouchi tayari alikuwa mahakamani mwezi Novemba mwaka jana kwa madai kuwa chama chake kilisaidia wanajihadi kusafiri hadi Iraq na Syria.

Kabla ya hapo, alihojiwa kuhusu madai ya ufujaji wa pesa kuhusiana na michango ya kigeni kwa shirika la usaidizi linalohusishwa na Ennahdha.

Ghannouchi ndiye kiongozi mashuhuri wa upinzani aliyekamatwa kufuatia unyakuzi wa rais Saied.

Ni miongoni mwa wapinzani zaidi ya 20 wa Saied waliokamatwa tangu Februari, wakiwemo mawaziri wa zamani na wafanyabiashara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.