Pata taarifa kuu

Bunge la Libya limemsimamisha kazi waziri mkuu wake mteule, Fathi Bashagha

Nairobi – Serikali hasimu ya Libya kupitia kwa bunge lake imempa wadhifa mpya waziri wake wa fedha, Osama Hamada na kwa sasa ndie waziri mkuu wa nchi hiyo baada ya Bunge hilo lenye makao yake mashariki mwa nchi hiyo kupiga kura ya kumsimamisha kazi , Fathi Bashagha.

Waziri mkuu wa Libya Fathi Bashagha amepoteza wadhifa wake serikalini
Waziri mkuu wa Libya Fathi Bashagha amepoteza wadhifa wake serikalini © Zoubeir Souissi, Reuters
Matangazo ya kibiashara

Bw Bashagha alichukua wadhifa huo mwaka jana lakini ameshindwa kuchukua nafasi ya waziri mkuu wa mpito mpinzani wa Serikali ya Makubaliano ya Kitaifa inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, Abdulhamid al-Ddeibah.

Bunge la mashariki lilisema mamlaka ya Bw al-Dbeidah yalimalizika mnamo Desemba 2021 baada ya uchaguzi wa kitaifa kuahirishwa.

Tangu wakati huo kumekuwa na makabiliano kati ya wafuasi wa watu hao wawili - hasa wakati Bw Bashagha alipojaribu na kushindwa kuingia Tripoli mwezi Mei mwaka jana.

Bunge la Libya mwaka jana lilimwapisha Fathi Bashagha kuwa waziri mkuu mpya huku waziri mkuu aliyekua madarakani Abdulhamid al-Dbeibah akikataa katakata kukabidhi hatamu za uongozi. 

Mivutano yao kuhusu nani alipaswa kuiongoza nchi hiyo tayari ilitishia kuzusha mapigano mapya au kulirejesha taifa hilo kwenye migawanyiko ya kimaeneo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.