Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Burkina Faso: Zaidi ya raia 30 wauawa katika shambulio jipya magharibi mwa nchi

Nchini Burkina Faso, shambulio jipya liliua takriban watu 33, wote wakiwa raia, Alhamisi, Mei 11, katika kijiji kilichoko magharibi mwa nchi.

Youlou ni wilaya inayopatikana katika kaunti ya Tcheriba katika mkoa wa Mouhoun nchini Burkina Faso.
Youlou ni wilaya inayopatikana katika kaunti ya Tcheriba katika mkoa wa Mouhoun nchini Burkina Faso. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Tukio hili lilitoea katika kijiji cha Youlou, katika kaunti ya Tcheriba, iliyoko katika mkoa wa Mouhoun. Tangazo hilo lilitolewa Jumamosi, Mei 13, na gavana wa eneo la Boucle du Mouhoun. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Babo Pierre Bassinga amelaani "shambulio la kikatili na la kinyama".

Shambulio hilo lilitokea siku ya Alhamisi mwendo wa saa kumi na moja jioni kwa saa za Burlina Faso. "Watu wenye silaha waliwalenga wananchi wenye amani wanaoshughulika na shughuli zao za bustani kwenye kingo za mto", amesema gavana ambaye ameripoti idadi kubwa ya watu waliouawa kwa muda, raia 33 waliuawa. Babo Pierre Bassinga amebainisha kuwa "hatua za usalama zinaendelea".

Vyanzo vya ndani ambavyo vimehojiwa na shirika la ha bari la AFP, vimethibitisha kuwepo, katika eneo hilo, kwa watu "waliojihami kwa silaha nzito", wanaozunguka kwenye pikipiki. Washambuliaji hawa waliwafyatulia risasi wakulima wa bustani bila kuchaguwa, vinasimulia vyanzo hivyo vinavyobainisha kuwa waathiriwa walizikwa siku ya Ijumaa.

Burkina Faso bado inalengwa mara kwa mara na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi, katika baadhi ya maeneo, hasa Mashariki, Katikati-Mashariki na Kaskazini, ambapo mashambulio kadhaa yalifanyika katika wiki za hivi karibuni, na kusababisha vifo vingi, hasa kati ya kikosi cha raia wanaosaidia jeshi na wanamgambo.

Ishara kwamba hali ya usalama bado ni tete, hali ya hatari iliyokuwepo tangu mwezi Machi katika mikoa 8 kwa jumla ya mikoa 13 ya nchi iliongezwa siku ya Ijumaa kwa miezi 6 na Bunge la kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.