Pata taarifa kuu

AU kuchukua udhibiti wa usalama Mashariki mwa DRC ?

NAIROBI – Umoja wa Afrika huenda ukalichukulia mikononi mwake swala la usalama katika eneo la mashariki mwa DRC wakati huu juhudi za kikanda zikiendelea huku mikanganyiko ikishuhudiwa kuhusu maamuzi ambayo yamekuwa yakichukuliwa.

Wanajeshi wa Kenya ambao ni sehemu ya kikosi cha jumuiya ya Afrika Mashariki nchini DRC
Wanajeshi wa Kenya ambao ni sehemu ya kikosi cha jumuiya ya Afrika Mashariki nchini DRC REUTERS - ARLETTE BASHIZI
Matangazo ya kibiashara

Mkataba wa Mfumo wa Addis Ababa, mchakato wa Nairobi, wa Luanda, utaratibu wa pamoja wa mkutano wa ukanda wa maziwa makuu, ni sehemu ya michakato mingi kuhusu hali ya usalama mashariki mwa DRC ambapo sasa inabidi kuongeza juhudu za nchi za Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) kutuma vikosi vyake.

Wataalamu wanaona hii ni sana viungo vikiwa vingi huharibu mchuuzi, na inahitaji ufafanuzi zaidi kabla ya kuongeza wanajeshi wengine.

Haja ya kuwepo uratibu imedhihirika katika mkutano wa viongozi wa ukanda wa maziwa makuu jijini Bujumbura nchini Burundi Jumamosi iliopita na Jumatatu katika mkutano wa Windhock nchini Namibia ambapo sasa wameamuwa kukutana tena chini ya usimamizi wa Umoja wa Afrika.

Marais wa nchi wanachama wa Muungano wa SADC, Mei 8, nchini Namibia.
Marais wa nchi wanachama wa Muungano wa SADC, Mei 8, nchini Namibia. © @SADC_News

Mkutano wa pande tatu utayoyakutanisha mashirika yote ya kikanda, SADC, EAC na ICGLR lengo ikiwa ni kupanga uratibu wa michakato iliopo na kukubaliano juu ya vikosi mbalimbali vya kikanda hususan vile vya ukanda wa Afrika mashariki vilivyo huko tangu Oktoba mwaka 2022, ambavyo serikali ya Kinshasa imekosoa ufanisi wake na sasa ujio wa vikosi vya SADC ambavyo mamlaka yake itakuwa ni kushambulia.

Wanajeshi wa EAC wanaopambana na makundi ya waasi mashariki ya DRC
Wanajeshi wa EAC wanaopambana na makundi ya waasi mashariki ya DRC AP - Ben Curtis

Umoja wa Afrika umekubaliana na pendekezo la kufanyika mkutano huo ambao hata hivyo haukueleza ni wapi na lini utafanyika, licha ya kuthitisha kuwa utafanyika kabla ya mwisho wa mwezi Mei kulingana na mjumbe wa umoja wa Afrika katika eneo la ukanda.

Makundi ya watu wenye silaha yameendelea kutatiza usalama wa raia mashariki mwa DRC
Makundi ya watu wenye silaha yameendelea kutatiza usalama wa raia mashariki mwa DRC AP - Moses Sawasawa

Mashariki mwa nchi ya DRC kumekumbwa na ghasia kutoka kwa makundi yenye silaha, hususan uwasi wa M23 ambao umeteka sehemu ya jimbo la Kivu Kaskazini. Na kwa karibu miaka 10, juhudi za kikanda zimekuwa zikikusanyika katika kujaribu kutatua mzozo huu

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.