Pata taarifa kuu

Muungano wa SADC kuwatuma wanajeshi wake Mashariki mwa DRC

NAIROBI – Muungano wa mataifa ya kusini mwa Africa, SADC, umekubaliana kutuma wanajeshi wake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo, kulinda amani na kurejesha utulivu kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara ya makundi ya waasi.

Marais wa nchi wanachama wa Muungano wa SADC, Mei 8, nchini Namibia.
Marais wa nchi wanachama wa Muungano wa SADC, Mei 8, nchini Namibia. © @SADC_News
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yaliafikiwa kwenye mkutano wa nchi wanachama wa muungano huo, lakini idadi kamili ya wanajeshi watakaotumwa haijawekwa wazi au kipindi ambacho wanajeshi hao watatumwa.

Wachambuzi wa siasa za DRC wanaona hatua hii haitakuwa na manufaa zaidi kama anavyoeleza Professa Dady Sale.

Wanakuja tu kwa sababu ya kuchunguza, kwa hii muda wanataka kukuja italeta shida tena zaidi kwa sababu hata kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki hatujui kama kilikuja kupigana na M23.
00:32

Prof. Dady Sale 9 5 23 kuhusu SADC

Baadhi ya majeshi kutoka nchi tatu za muungano wa SADC, kutoka Afrika Kusini, Tanzania na Malawi, tayari yanaendelea kuhudumu mashariki mwa DRC tangu mwaka 2013, chini ya mwavuli wa MONUSCO.

Wikendi iliyopita, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, alihutubia mkutano nchini Burundi wa mataifa ya Afrika yaliyotia saini mkataba wa 2013 wa kukuza utulivu na usalama nchini DRC, na kutoa himizo kwa viongozi hao kuweka mara dufu juhudi zao katika kuleta amani kwenye eneo hilo.

Ni wakati wa ghasia kukomesha. Narudia wito wangu kwa makundi yote yenye silaha -- wekeni chini silaha zenu mara moja, alisema Guterres.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi kuanzia Jumanne, Mei 9, anaanza ziara ya siku nne nchini Botswana, nchi ambayo ni makao makuu ya muungano wa SADC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.