Pata taarifa kuu

Viongozi wa nchi za maziwa makuu kukutana Jumamosi jijini Bujumbura

NAIROBI – Vionogzi wa ukanda wa maziwa makuu wanakutana hapo kesho Jumamosi jijini Bujumbura kufanya tathmini ya maendeleo ya makubaliano ya mfumo wa amani na ushirikiano wa Jamhuru ya Kidemkorasia ya Congo na ukanda yaliotiwa saini jijini Addis Ababa miaka 10 iliopita.

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, akiteta jambo na katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dr Peter Mathuki. 04 / 02 / 2023
Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, akiteta jambo na katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dr Peter Mathuki. 04 / 02 / 2023 Β© Jumuiya
Matangazo ya kibiashara

Maandalizi ya mkutano wa 11 wa utaratibu wa ufuatiliaji wa mfumo wa makubaliano ya amani, usalama na ushirikiano kwa DRC na ukanda, yamekamilika, ambapoΒ  wakuu wa nchi na Serikali watakutana mbele ya washirika wao wakiongozwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres. Jiji la Bujumbura limepambwa kwa rangi ya sherehe, kuwapokea viongozi hao.

Mkutano huo umetanguliwa na ule wa baraza la mawaziri wa mataifa hayo uliofanyika jana jijini Bujumbura.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres ni miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres ni miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo AP - Khalil Senosi

Katika ufunguzi wa baraza hili la mawaziri wa nchi zilizotia saini mkataba wa mfumo wa Addis Ababa, wazungumzaji wote, ikiwa ni makatibu wakuu wa SADC, ICGLR na mwakilishi mkuu wa umoja wa Afrika katika ukanda wa maziwa makuu wamekutana juu ya haja ya kufufua mikataba hiyo ili Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na eneo hilo kurejesha amani.

Mwakilishi wa umoja wa Mataifa katika eneo la Maziwa Makuu Huang Xia alidokeza kuwa mkutano huu unafanyika wakati mgogoro mkubwa mashariki mwa Kongo ukiendelea kushuhudiwa kama vile kuendelea kwa waasi wa M23, ADF, FDLR, Red Tabara na makundi mengine ya wenyeji ambayo yanaendeleza ukosefu wa usalama na mateso yasiyovumilika ya raia.

Waasi wa M23 wamekataa kuondoka katika maeneo wanayokalia licha ya kutakiwa kufanya hivyo na viongozi wa nchi za EAC
Waasi wa M23 wamekataa kuondoka katika maeneo wanayokalia licha ya kutakiwa kufanya hivyo na viongozi wa nchi za EAC Β© EAC

Mvutano kati ya baadhi ya nchi katika eneo hilo unaendelea na kusababisha kuongezeka kwa matamshi ya chuki, uchochezi wa ghasia na kuzidisha hali ya wasiwasi.

Kwa bahati nzuri, eneo hilo limejipanga ili kupunguza hali ya wasiwasi na kutafuta suluhu la changamoto nyingi za kijeshi na kibinadamu, aliongeza Huang Xia, mwakilishi. wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Maziwa Makuu.

Baraza hili la Mawaziri lilitanguliwa na kikao cha siku 2 cha Kamati ya Usaidizi wa Kiufundi cha maandalizi ya mkutano wa utaratibu wa udhibiti wa kikanda (ROM) ambao ulizingatia pointi 2, ambazo ni uchunguzi na kupitishwa kwa mradi. ya makubaliano ya mfumo, uchunguzi na kupitishwa kwa rasimu ya taarifa ya mwisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.