Pata taarifa kuu

Sudan: Janga la kibinadamu laikumba nchi wakati huu mapigano yakiendelea

NAIROBI – Umoja wa mataifa umetaka kupewa hakikisho kutoka kwa majenerali wawili mahasimu nchini Sudan, kuwa msaada wa kibinadaamu unaohitajika mno, unasafirishwa na kuwafikia waathiriwa wa mapigano.

Moshi mjini Khartoum kufuatia mapigano mapya katika mji mkuu wa Sudan Mei 3, 2023.
Moshi mjini Khartoum kufuatia mapigano mapya katika mji mkuu wa Sudan Mei 3, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Wito wa Guterres umekuja baada ya malori sita yaliyokuwa yanapeleka msaada eneo la Darfur kuporwa.

Katibu mkuu wa umoja huo Antonio Guterres akizungumza na waandishi kwa njia ya video, ameonya kuhusu janga la kibinadamu kufuatia vita vinavyoendelea.

La kusikitisha, naona hali imezidi kuharibika, na msaada wa kibinadaam unaohitajika zaidi haufai kukatizwa na unahitaji usalama kuwafikia walengwa. UN umekuwa ukifanya kazi karibu na IGAD na AU ila mikataba yote ya usitishwaji mapigano haijaweza kudumu, amesema Guterres.
00:43

Antonio Guterres, katibu mkuu wa UN, kuhusu msaada wa kibinadamu 3 5 2023

Aidha Guterres amesisitiza haja ya pande zinazohasimiana kutafuta namna ya haraka ya kumaliza mzozo huo akisema jamii ya kimataifa inaunga mkono juhudi za kuleta amani.

Jamii ya kimataifa imekuja pamoja, mazungumzo ya kisiasa yanahitajika kufanyika na hatimaye kurejeshwa kwa utawala wa kiraia, Guterres ameongeza.
00:25

Antonio Guterres, Katibu mkuu wa UN, kuhusu hali ya kisiasa 3 5 23

Ujumbe wa UN

Wakati huo huo, Martin Griffiths, mkuu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa,  aliwasili Jumatano katika Bandari ya Sudan kwenye ufuo wa Bahari Nyekundu kwa misheni ya dharura ya kutafuta njia za kuleta afueni kwa mamilioni ya raia wa Sudan, ambao hawawezi kutoroka.

Bado tutahitaji makubaliano na mipango ya kuruhusu usafirishaji wa wafanyikazi na vifaa, amewaambia waandishi wa habari kupitia video kutoka Bandari ya Sudan.

Mapigano yameendelea kuripotiwa jijini Khartoum licha ya kuwepo makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano, mkataba mpya wa amani ukiongezewa muda wa juma moja kuanzia Mei 4 hadi 11.

Rais wa Eritrea, Isaias Afwerki ametangaza nchi yake kufungua mipaka kwa raia wa Sudan na  nchi zingine kwa wanaokimbia mapigano nchini Sudan, pamoja na kutoa msaada kadri ya uwezo wao, wakati pia akisisitiza haja ya kumaliza mara moja mzozo unaoendelea nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.