Pata taarifa kuu

Mazungumzo ya serikali ya Ethiopia na kundi la OLA yakosa mwafaka: Serikali

NAIROBI – Mazungumzo ya awali kati ya serikali ya Ethiopia na kundi la waasi wa Oromo Liberation Army (OLA),  yamekamilika Jumatano, Mei 3, bila kufikia makubaliano yoyote, kwa mujibu wa Addis Ababa.

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed AP - Mulugeta Ayene
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya yalianza wiki iliyopita nchini Tanzania, katika mkutano ambao msemaji wa wa OLA, Odaa Tarbii, ameyaeleza kama mazungumzo yenye nia ya kuanzisha msingi wa majadiliano ya kina zaidi.

Kundi la OLA, vuguvugu la waasi wenye silaha kutoka eneo la Oromia nchini Ethiopia, limekuwa likipambana na serikali ya Addis Ababa tangu lilipojitenga mwaka 2018 kutoka kwa Oromo Liberation Front (OLF) wakati kundi hilo lilipoachana na mapambano ya silaha.

Kwa kiasi kikubwa mazungumzo yamekuwa ya kujenga, kwa bahati mbaya, haikuwezekana kufikia makubaliano juu ya baadhi ya masuala wakati wa duru hii ya mazungumzo," huduma ya mawasiliano ya serikali ya Ethiopia ilisema katika taarifa iliyotolewa Jumatano.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa pande zote mbili zimekubaliana kuhusu haja ya kuendelea na mazungumzo kwa lengo la kusuluhisha kabisa mgogoro uliopo kwa amani.

Tangu kundi la OLA, kujitenga na lile la  OLF Na kuanza mapigano, msururu wa makundi yenye silaha huko Oromia yameibuka yakidai kuwa sehemu yake, lakini hayana mkataba wa kuwaunganisha.

Oromia inazunguka Addis Ababa na ni eneo kubwa na lenye watu wengi zaidi Ethiopia, na imekumbwa na mauaji ya kikabila katika miaka ya hivi karibuni yaliyotekelezwa na makundi yasiyojulikana.

Mara kwa mara serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed, imekuwa ikishutumu kundi hili kwa kuhusika na mauaji, madai ambayo kundi hilo linakanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.