Pata taarifa kuu

Guterres anazuru Kenya kabla ya kuelekea Burundi kujadili usalama mashariki mwa DRC

NAIORBI – Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewasili nchini Kenya ambapo amepokelewa na waziri wa mambo ya kigeni katika taifa hilo la Afrika Mashariki Alfred Mutua, akitarajiwa pia kufanya mazungumzo na mkuu wa nchi, Rais William Ruto.

António Guterres , Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa
António Guterres , Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa AP - Lujain Jo
Matangazo ya kibiashara

Guterres, anatarajiwa kuwa miongoni mwa viongozi watakaohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za ukanda mjini Bujumbura, kujadiliana kuhusu hali ya usalama mashariki mwa DRC mwishoni mwa wiki hii.

Mkuu huyo wa UN, atawasili nchini Burundi, akitokea nchini Kenya, baada yake kuwa na mazungumzo na rais wa Kenya, William Ruto, ambapo watajadiliana kuhusu hali ya usalama nchini Sudan na DRC.

Mbali na Sudan, akiwa nchini Kenya, pia anatarajiwa kujadiliana na mwenyeji wake kuhusu hatua zinazoendelea kuchukuliwa kuhusu kudhibiti usalama mashariki mwa nchi ya DRC.

Baada ya hapo, Guterres atatarajiwa nchini Burundi, ambako atakutana na rais Evariste Ndayishimiye, ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo watajadiliana kuhusu hali ya usalama mashariki mwa DRC kabla ya kushiriki kikao na viongozi wengine wa ukanda.

Ziara yake inakuja wakati huu ambapo, wakuu wa nchi wanatarajia kujadili hatua zilizochukuiliwa kuhusu mkataba wa amani wa Angola, pamoja na wajibu wa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambavyo viko nchini Congo kwa miezi kadhaa sasa.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Kenya, Alfred Mutua
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Kenya, Alfred Mutua © Wizara ya mambo ya nje ya Kenya

Mkutano huu wa wakuu wa nchi za maziwa makuu, utafanyika huku makundi ya waasi likiwemo lile la M23, lililotakiwa kuachia maeneo inayoyakalia mashariki mwa nchi hiyo, yakiendelea kutatiza usalama kwa kutekeleza mauaji ya kiholela dhidi ya raia.

Wakati huu mkuu huyo wa umoja wa mataifa akiwa nchini Kenya kujadili suala la mapigano nchini Sudan, kiongozi mwengine wa ngazi ya juu katika umoja huo Martin Griffiths amethibitisha kuwasili nchini Sudan.

Inaaminika kuwa uwepo wa kiongozi huyo unalenga kujadili mbinu za kuwafikishia misaada ya kibindamu mamilioni ya raia waliokwama nchini Sudan kutokana mapigano yanayoendelea kati ya makundi mawili ya kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.