Pata taarifa kuu

WHO yahofia maafa zaidi nchini Sudan kutokana na mlipuko wa magonjwa

NAIROBI – Shirika la afya duniani WHO, limesema huenda vifo zaidi vikaripotiwa nchini Sudan, kutokana na mlipuko wa magonjwa na kusitishwa kwa huduma muhimu, kufutia mapigano hayo.

Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus AP - Salvatore Di Nolfi
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema ni asilimia 16 pekee ya huduma za matatibu ndizo zinatolewa kwa sasa nchini Sudan

Kando na majeruhi na mzozo wenyewe , WHO, inatarajia kwamba kutakuwepo na vifo zaidi vinavyotokana na mlipuko wa magonjwa, ukosefu wa maji na chakula pamoja na kuvurugika kwa huduma muhimu ikiwemo chanjo, Amesema Ghebreyesus.
00:38

Mkurugezi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus

Jeshi nchini Sudan, limeendelea kushambulia wapiganaji wa RSF  kupitia mashambulizi ya anga, jijini Khartoum, licha ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyofanikishwa na Marekani

Licha ya jeshi Jumatano kutangaza kuwa tayari kushiriki mazungumzo ya amani, jijini Juba, kumeripotiwa mashambulizi kadhaa yaliowalenga wapiganaji wa RSF, leo ikiwa ni siku ya 13 tangu wanajeshi wanaunga mkono serikali kuanza kujibu mashambulizi kutoka kwa wapiganaji wa RSF.

Juhudi za kimataifa na kikanda zimeendelea kutolewa kujaribu kupatanisha pande hasimu tangu april  15,  kati ya Kiongozi wa kijeshi Abdel Fattah al-Burhan na aliyekuwa naibu wake Mohamed Hamdan Daglo, lakini juhudi hizo zimekosa kuzaa matunda.

Burhan ameitikia wito wa IGAD wa kufanya mazungumzo  na kuongeza muda wa kusitisha mapigano kwa saa 72 zaidi, huku kundi la RSF likisalia kimya kuhusu pendekezo hilo.

Kwa mjibu wa wizara ya afya nchini Sudan, watu 512 wamefariki tangu kuanza kwa mapigano hayo, wengine 4, 193, wakisalia na majeraha, japo huenda idadi ya vifo ikawa juu zaidi.

Nayo Umoja wa Mataifa  imesema zaidi ya watu 3,500 wakiwemo raia wa Uturuki, wamewasili nchini Ethiopia, wakitoroka mapigano ya Sudan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.