Pata taarifa kuu

Smart Africa: Upatikanaji wa mitaji sio shida kwa bara la Afrika

Kwa mujibu wa takwimu za bara la Afrika, biashara ndogo na zile za kati zinavutia uwekezaji wa karibu dola za Marekani bilioni 5 kwa mwaka, huku asimilia 50 ya biashara hizo zikiwa Nigeria.

Mkurugenzi wa Smart Afrika, Lacina Koné, akitia saini moja ya mikataba ya ushirikiano katika kukuza teknolojia na benki ya maendeleo ya Afrika.
Mkurugenzi wa Smart Afrika, Lacina Koné, akitia saini moja ya mikataba ya ushirikiano katika kukuza teknolojia na benki ya maendeleo ya Afrika. © SmartAfrica
Matangazo ya kibiashara

Wadau wanasema nchi za Afrika lazima ziongeze uwekezaji katika upatikanaji wa huduma ya intaneti kwa raia wake, kama zinataka kufikia kwa haraka maendeleo endelevu.

 

Kidole kimoja hakivunji chawa, ni mfano uliotolewa na mkurugenzi wa taasisi ya Smart Africa, Lacina Koné, ambaye anakiri kuwepo kwa changamoto ya nchi za Afrika kila mmoja kutaka kufanya jambo la maendeleo ya teknolojia peke yake.

 

Koné, anasema kwa bishara ndogo na za kati kukua, nchi zinapaswa kuondoa vikwazo vya kibiashara na kutengeneza sera nzuri zitakazovutia uwekezaji barani Afrika.

 

Utafiti unaonesha asilimia 90 ya biashara zilizoanzishwa hazikufa kwasababy ya kifedha, ni kwasababu ya kukosa mafunzo, uongozi na maendeleo ya biashara. Jambo la pili katika ngazi ya kidunia, pesa iko ili itumike…kwahiyo fedha kwangu mimi ni kama mvua na kama tunavyojua ili mvua inyeshe unahitaji vitu kadhaa kama mawingu na mawingu hayo ni mazingira rafiki ya sheria zitakazovutia ambazo nchi zetu lazima zifanyie kazi ili kumvutia muwekezaji. Alisema Lacina Koné.

 

Kuhusu ushiriki wa sekta binafsi, Koné anasema sekta hii kile ambacho haipendo ni kutotabirika kwa mazingira ya ufanyaji biashara na hasa kupitia teknolojia na kwamba ni lazima sera za nzi za Afrika zihuishwe kuleta urari wa kibiashara.

Kama kweli tunataka sekta binafsi itumie fursa ya uwepo wa idadi ya watu bilioni 1 na laki 5 barani Afrika na tuna nchi 50 ambazo nchi zote 50 zinamifumo tofauti ya usimamizi..nadhani sote tunajua kwamba lazima tuwajibike katika kuhuisha mifumo yetu, kwahivyo nadhani kwangu mimi hii ndio changamoto kubwa. Aliongeza Koné. 

Kwa kuwa upatikanaji wa fedha sio shida kwa bara la Afrika, Smart Afrika kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo serikali ya Luxembourg na kampuni ya uwekezaji mitaji ya Bamboo Capital Partners, wameanzisha mfuko unaofahamiaka kama Block Smart Afrika, kuwawezesha wajasiriamali katika sekta ya teknolojia.

 

Winnie Mwangi, mkurugenzi wa uwekezaji kutoka kampuni ya Bamboo Capital Partners ya nchini Kenya, anasema wao wanaamini katika teknolojia kama mkombozi wa changamoto zinazoshuhudiwa barani Afrika na hasa kwenye sekta za afya, elimu, kilimo na uhuishwaji wa kifedha.

Winnie anasema mfuko huu ni wakipekee kwasababu ni ushirikiano kati ya sekta binafsi na uma na kwamba kwasasa tayari serikali ya Ivory Coast imeshawekeza kwenye mfuko huu.

Mwishowe utagundua unahitaji mwekezaji ambaye atakubali hatari ya biashara yenyewe hasa katika kipindi ambacho biashara inahitaji uwekezaji. Kwahiyo kuna tofauti kubwa sana kati ya uwekezaji wakati biashara inapoanza na baadae….changamoto kubwa sana katika hii biashara hii ya teknolojia ni wapi utapata fedha katika hatua za awali kabisa, lakini pia wapi pakupata msaada za ziada, mbali na ufadhili wa kifedha. Alisema Winnie Mwangi.

 

Teknolojia dijiti inatoa fursa za ukuaji wa kiuchumi kwa bara la Afrika ikiwa ni pamoja na kutengeneza ajira, upatikanaji wa huduma za uma, kuongeza uzalishaji na ubunifu.

 

Hata hivyo bado kuna changamoto, idadi ndogo ya watu waliounganishwa na huduma ya intaneti hasa vijijini pamoja na matumizi hafifu ya teknolojia katika maeneo yaliyounganishwa bado ni shida kwa watu masikini, wanawake na biashara ndogondogo.

 

Ongezeko la hatari za kimtandao na kutokuwepo kwa ulinzi wa taarifa za watumiaji, zimeleta changamoto mpya kwa biashara, Serikali na hata watu wa kawaida.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.