Pata taarifa kuu

Mataifa ya Chad na Sudan Kusini kupokea idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Sudan

NAIROBI – Umoja wa mataifa unasema kuwa zaidi ya 270,000 wanaweza kutoroka mapigano nchini Sudan kutafuta hifadhi katika mataifa ya Sudan Kusini na Chad

Raia wa Sudan wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji na chakula
Raia wa Sudan wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji na chakula REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Shirika la kutetea haki za wakimbiza katika umoja wa mataifa nchini Chad limethibitisha kuwasili kwa raia elfu ishirini  wameingia nchini humo wakitokea Sudan, idadi hiyo iktarajiwa kufikia laki moja.

Hali ni sawa kwa upande wa Sudan Kusini ambayo na yenyewe inasema kuwa inatarajia kupokea wakimbizi elfu 45 watakaovuka mpaka wakitokea Sudan ya juu.

Aida Sudan Juba pia inatarajiwa kuwapokea wakimbizi 125,000 waliotoroka nchini humo kuelekea nchini Sudan wakati wa mapigano.

Licha ya hayo, shirika la missada la umoja wa mataifa limesema kwamba limelazimika kukatiza shughuli zake nchini Sudan kutokana na mapigano yanayoendelea kati pande mbili za kijeshi.

Wafanyikazi watano wa kutoa misaada wameripotiwa kuawua tangu tarehe 15 Aprili .Shirika la mpango wa chakula duniani WFP tayari limesitisha shughuli zake nchini Sudan.

Haya yanajiri wakati huu mataifa mbali mbali yakiendelea kuwaondoa raia wake nchini Sudan, mataifa ya Afrika kama vile Kenya yakiwa yamepokea sehemu ya kwanza ya raia wao waliokuwa wanaishi nchini humo.

Raia wa Sudan kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa chakula, maji na dawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.