Pata taarifa kuu

Sudan: Wito wa kusitishwa kwa mapigano waendelea kutolewa

NAIROBI – Nchini Sudan wito na shinikizo za kidiplomasia zinaendelea kuongezeka kwa pande hasimu za kijeshi katika taifa hilo kusitisha mapigano ambayo kwa sasa yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 300 katika kipindi cha wiki moja sasa.

Wito wa kusitishwa kwa mapigano nchini Sudan wamendelea kutolewa.
Wito wa kusitishwa kwa mapigano nchini Sudan wamendelea kutolewa. AP - Marwan Ali
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wa jeshi la Sudan wamekuwa wakipigana na vikosi maalum vya Rapid Support Forces (RSF), raia wakionekana kuathirika katika makabiliano hayo.

Haya yanajiri wakati huu Umoja wa Mataifa, Marekani na mataifa mengine yameendelea kutoka shinikizo la kutaka kusitishwa kwa vita hivyo kwa muda wa siku tatu kama njia moja ya kuadhimisha sikukuu ya Waislamu ya Eid al-Fitr.

Antonio Guterres ni katibu mkuu wa umoja wa mataifa.

“Kwa kuipa kipaumbele, naomba kusitishwa kwa mapigano kwa takriban siku tatu kusherekea siku tatu ya idd Fitr, ili kuwaruhusu raia ambao wamekwama katika maeneo ya mapigano kuondoka, kutafuta huduma za matibabu, chakula na bidhaa zengine za msingi.” ameeleza Guterres.

00:27

Antonio Guterres Kuhusu Sudan

RSF inasema imekubali kusitisha mapigano ya saa 72 kwa misingi ya kibinadamu, awali wapiganaji hao walikuwa wametoa kauli sawa na hii japokuwa mapigano yaliripotiwa kuendelea. Majaribio mawili ya awali ya kusitisha mapigano yalishindwa kuzaa matunda.

Licha ya RSF kutoa ahadi ya kusitishwa kwa mapigano katika kipindi cha saa 72, Kiongozi wa serikali ya kijeshi nchini Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, awali alitupilia mbali uwezekano wa kuwepo kwa mazungumzo na vikosi vya RSF.

Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikitoa wito kwa pande zinazopigana nchini humo kutoa nafasi ya kwa raia walioathirika na mapigano hayo kupata msaada wa kibinadmu ikiwemo kupokea huduma za matibabu.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa kati ya watu 10,000 hadi 20,000 - wengi wao wakiwa wanawake na watoto wamekimbia Sudan kutokana na mapigano makali huko ili kutafuta usalama katika nchi jirani ya Chad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.