Pata taarifa kuu

Sudan: Mapigano yaua zaidi ya watu 400, kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni

Mapigano yaliyozuka katikati ya mwezi wa Aprili nchini Sudan tayari yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 400 na wengine zaidi ya 3,500 kujeruhiwa, Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Aprili 21, 2023. "Watu 413 wamefariki na watu 3,551 wamejeruhiwa," Msemaji wa WHO Margaret Harris amesema katika mkutano wa kila siku na waandishi wa habari huko Geneva.

Makabiliano yanaendelea kuripotiwa nchini Sudan
Makabiliano yanaendelea kuripotiwa nchini Sudan AP - Marwan Ali
Matangazo ya kibiashara

Tangu Aprili 15, mapigano hayo ambayo yamejikita zaidi katika mji mkuu Khartoum na katika jimbo la Darfur, yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 400 na wengine 3,500 kujeruhiwa. Kwa wasiwasi mkubwa, jumuiya ya kimataifa imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano siku ya Ijumaa, kwa ajili ya kumalizika kwa mfungo mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Wakati huo huo mapigano makali yanaendelea nchini Sudan siku ya Ijumaa, Aprili 21, siku ya saba ya mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo, licha ya wito mwingi wa kusitisha mapigano, huku wakaazi wengi wakisherehekea Eid-el-Fitr, kuashiria kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Kwa wakati huu, "watu 413 wamekufa na watu 3,551 wamejeruhiwa," msemaji wa Shirika la Afya Ulimwenguni Margaret Harris amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Geneva.

Msemaji wa UNICEF, James Elder, amemwambia kwamba "angalau watoto 9 waliuawa katika mapigano hayo, na zaidi ya watoto 50 wameripotiwa kujeruhiwa".

Milio ya risasi na mashambulio ya anga yametikisa mji mkuu Khartoum usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa, kisha asubuhi, kama ilivyokuwa kila siku tangu Aprili 15 na kuanza kwa mapigano haya, ambayo yalijikita zaidi mji wa Khartoum na mkoa wa Darfur.

Hata hivyo, mawasiliano ya kidiplomasia yameongezeka tangu siku ya Alhamisi, Jenerali Abdel Fattah Al-Bourhane, mkuu wa jeshi na kiongozi mkuu wa Sudan tangu mapinduzi ya mwaka 2021, almetangaza kwamba aliwasiliana na viongozi wa kikanda, hasa rais wa Sudan Kusini, rais wa Ethiopia na viongozi wengine wengi tu, ikiwa ni pamoja Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.