Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Watu 10 wa familia moja wameuawa na watu wenye silaha

NAIROBI – Watu 10 kutoka familia moja wameuawa katika mji wa Pietermaritzburg nchini Afrika Kusini, baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha. 

Mji wa Pretoria Afrika Kusini
Mji wa Pretoria Afrika Kusini © gettyImages
Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa polisi wanasema wanachunguza kilichosababisha watu hao wa familia kupigwa risasi na kuawa, katika shambulio wanalosema ni la kushtukiza. 

Wanawake saba na wanaume watatu, ndio waliouawa katika tukio hilo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara inayohusika na masuala ya polisi. 

Waziri wa masuala ya Polisi, Bheki Cele akizungumza akiwa mkoani KwaZulu-Natal kulikofanyika mauaji hayo, amesema uchunguzi unaendelea lakini akaeleza hali kuwa mbaya na ya kusikitisha. 

Mwezi Januari, tukio lingine kama hili, liliripotiwa ambapo watu wenye silaha waliwauwa watu wanane na kuwajeruhi wengine watatu wakati wa sherehe ya kuzaliwa katika mji wa Gqeberha. 

Afrika Kusini inasalia mojawapo ya nchi duniani, yenye visa vingi vya mauaji vinatokana na watu kuuawa kwa kupigwa risasi au kuuawa, huku takwimu zionesha kuwa watu karbu Elfu 20 huawa kila mwaka. 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.