Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Mauaji ya watu sita Afrika Kusini: Uchunguzi waanzishwa kubaini wahusika

Uchunguzi umefunguliwa baada ya watu sita kuuawa kwa kupigwa risasi siku ya Jumatano katika kitongoji cha wafanyakazi karibu na Cape Town katika kile kinachoonekana kama ulipizaji kisasi, polisi imebaini.

Mwanamke ambaye ni ndugu wa mmoja wa waathiriwa waliopigwa risasi akilia huku maafisa wa polisi wa Afrika Kusini wakikataa kumruhusu kuvuka kizuizi cha polisi na kuingia katika eneo la uhalifu, huko Soweto, Afrika Kusini, Julai 10, 2022.
Mwanamke ambaye ni ndugu wa mmoja wa waathiriwa waliopigwa risasi akilia huku maafisa wa polisi wa Afrika Kusini wakikataa kumruhusu kuvuka kizuizi cha polisi na kuingia katika eneo la uhalifu, huko Soweto, Afrika Kusini, Julai 10, 2022. © AFP - IHSAAN HAFFEJEE
Matangazo ya kibiashara

Washambuliaji kadhaa wenye silaha waliegesha gari lao asubuhi mbele ya nyumba inayopatikana katika mjii wa Ocean View, kwenye rasi ya kitalii ya Cape Town. Waliingia na kuanza kufyatua risasi. Wanaume watano, wenye umri wa kati ya miaka 20 na 50, waliuawa. Wa sita, aliyepigwa risasi na kujeruhiwa, alipelekwa hospitalini ambako alifariki, inasema taarifa.

Uchunguzi umefunguliwa kwa mauaji, polisi wakishuku, kulingana na ushahidi wa kwanza uliokusanywa papo hapo, 'ulipizaji kisasi' kuhusiana na shughuli za magenge". Hakuna mtu aliyekamatwa na polisi wamewataka mashahidi kujitokeza.

Uchunguzi, katika eneo hili hasa lenye "lenye idadi ndogo kabisa ya maafisa wa polisi", una hatari ya kuwa ngumu zaidi kutokana na kwamba "kamera za usalama (CCTV) zilizimwa" wakati wa shambulio hilo, madhara ya kukatika kwa umeme mara kwa mara katika miezi ya hivi karibuni nchini, kimesema  katika taarifa kwa vyombo vya habari chama cha Democratic Alliance (DA), chama kikuu cha upinzani ambacho kinaongoza jimbo hili kusini mwa nchi.

Mji wa Ocean View uliundwa chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi ili kuhifadhi ufuo wa kuvutia kati ya bahari na milima kwa Wazungu. Mnamo mwaka 1968, serikali ya ubaguzi ilijenga, ndani ya nchi, makazi ya watu mchanganyiko wanaitwa "coloured" waliohamishwa kutoka kwa bandari za uvuvi na maeneo jirani ya mapumziko kwenye ufukwe wa bahari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.