Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Afrika Kusini: Mfungwa mtoro aliyejifananisha na maiti arejeshwa gerezani

Mfungwa muuaji nchini Afrika Kusini ambaye alitoroka jela baada ya maiti iliyochomwa moto kugunduliwa katika chumba alikokuwa anazuiliwa amesafirishwa kutoka Tanzania ambako alikamatwa wiki iliyopita, serikali ya Afriika Kusini imetangaza leo Alhamisi. Serikali imekuwa ikisumbuliwa na tukio hili baya kwa wiki kadhaa.

Polisi wa Afrika Kusini. Baada ya kukamatwa nchini Tanzania, mhalifu huyo "aliwekwa rumande" usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa katika gereza lenye ulinzi mkali karibu na Johannesburg.
Polisi wa Afrika Kusini. Baada ya kukamatwa nchini Tanzania, mhalifu huyo "aliwekwa rumande" usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa katika gereza lenye ulinzi mkali karibu na Johannesburg. Mike Hutchings/Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Tunaweza kuthibitisha kwamba waliotoroka wameletwa kutoka Tanzania hadi Afrika Kusini," Waziri wa Sheria Ronald Lamola amesema, akimzungumzia Thabo Bester na mwanamke anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi, walikamatwa pamoja siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita. Thabo Bester, aliyepewa jina la utani "mbakaji wa Facebook" kwa kuwavutia waathiriwa wake kupitia mtandao huu wa kijamii, alihukumiwa mwaka 2012 kifungo cha maisha jela kwa mauaji na ubakaji.

Mnamo mwezi Mei 2022, maiti iliyoteketea kwa moto ilipatikana katika chumba chake katika gereza la kibinafsi huko Bloemfontein. Kwa hiyo mamlaka ya magereza iliamini kwamba Bw. Bester alijiuwa kwa kujichoma moto akiwa mbaroni. Lakini kwa kweli alikuwa ametoroka: mwishoni mwa mwezi Machi, polisi ilifichua kuwa vipimo vya DNA vilionyesha kuwa mwili uliopatikana kwenye chumba chake haukuwa wake.

Baada ya kukamatwa nchini Tanzania, mhalifu huyo "aliwekwa rumande" usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa katika gereza lenye ulinzi mkali karibu na Johannesburg, Ronald Lamola amesema leo Alhamisi wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Cape Town, akiongeza kuwa mwandani wake atawasilishwa kwa jaji wakati wa mchana.

Babake mwanamke huyo ni mmoja wa watu wanne waliokamatwa kuhusiana na kisa hicho katika siku za hivi majuzi. Alishtakiwa mapema wiki hii kwa mauaji, kuhusiana na mtu huyo aliyepatikana amekufa katika chumba cha gereza cha Bester.

Kesi hii isiyo ya kawaida na mbaya imekuwa ikigonga vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari vya Afrika Kusini tangu wiki iliyopita. Siku ya Jumatano, msemaji wa rais Cyril Ramaphosa alisema mkuu wa nchi "anasumbuliwa" na kutoroka muuaji huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.