Pata taarifa kuu

Katibu mkuu wa UN, Antonio Guterres anazuru Somalia

NAIROBI – Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amewasili jijini Mogadishu kuaanza ziara yake nchini Somalia, nchi inayokabiliwa na changamoto za kiusalama na mabadiliko ya tabia nchi.

Katibu mkuu wa UN, Antonio Guterres yuko jijini  Mogadishu kwa ziara
Katibu mkuu wa UN, Antonio Guterres yuko jijini Mogadishu kwa ziara © somalia government official
Matangazo ya kibiashara

Picha zilizochapishwa katika ukurasa wa waziri wa mambo ya kigeni wa Somalia Abshir Omar Huruse, zimemuonyesha kiongozi huyo wa UN akilakiwa nchini humo na viongozi wengine.

Somalia imeweka vizuizi vya usalama jijini Mogadishu kutokana na  ziara hiyo ambayo haikutangazwa, huku barabara nyingi zikiwa zimefungwa, na usafiri wa umma ukitatizika.

Kuwasili kwa Guterres kunakuja wakati huu nchi hiyo ikikumbwa na janga la ukame ambalo limewafanya wengi kukabiliwa na njaa, huku serikali pia ikiwa inaendelea na mapambano dhidi ya makundi ya wanajihadi nchini humo.

Umoja wa Mataifa umezindua ombi la dola bilioni 2.6 kwa ajili ya msaada wa kibinadamu kwa taifa hilo lenye matatizo la Pembe ya Afrika, lakini kwa sasa linafadhiliwa kwa asilimia 13 pekee.

Misimu mitano ya kuchelewa kwa mvua  katika baadhi ya maeneo ya Somalia pamoja na Kenya na Ethiopia imesababisha ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo minne, na kuangamiza mifugo na mazao na kuwalazimu watu wasiopungua milioni 1.7 kutoka makwao kutafuta chakula na maji.

Umoja wa Mataifa unasema takriban nusu ya raia nchini Somalia watahitaji msaada wa kibinadamu mwaka huu, huku milioni 8.3 wakiathiriwa na ukame.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.