Pata taarifa kuu

Guterres ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuisaidia Somalia

NAIROBI – Katibu mkuu wa Umoja Antonio Guterres, ametoa wito kwa mara nyingine kwa jumuiya ya kimataifa kuisaidia Somalia ambayo inakabiliwa na janga la kibinadamu lililosababishwa na ukame pamoja na mashambulio ya makundi ya kijihadi.

Katibu mkuu wa UN Antonio Guterres akiwa na rais wa Somali Hassan Sheikh Mohamoud wakati wa ziara ya mkuu wa UN nchini Somalia
Katibu mkuu wa UN Antonio Guterres akiwa na rais wa Somali Hassan Sheikh Mohamoud wakati wa ziara ya mkuu wa UN nchini Somalia REUTERS - FEISAL OMAR
Matangazo ya kibiashara

Katika kikao cha pamoja na mwenyeji wake rais Hassan Sheikh Mohamud, Guterres ameeleza kuwa ziara yake inaonyesha mshikamano wake na taifa hilo ambalo raia wake milioni tano wanakabiliwa na baa la njaa na changamoto ya kiusalama.

Aidha ameiomba jamii ya kimataifa kuisaidia kuafikia lengo lake la dola za Marekani bilioni 2.6 kwa ajili ya misaada ya kibindamu, Guterres akisema UN imefanikiwa kupata asilimia 15 ya kiwango hicho.

Ziara yake imekuja wakati huu idadi kubwa ya raia wa Somalia wakiwa wanakabiliwa na ukosefu wa chakula huku pia serikali ya Mogadishu ikiwa mbioni kukabiliana na makundi ya wanajihadi wanaotatiza usalama.

Hii ni ziara ya kwanza ya mkuu huyo wa UN tangu mwezi Machi mwaka wa 2017 ambapo atazuru pia kambi za wakimbizi kabla ya kuhitimisha ziara yake hapo kesho.

Guterres awali alikuwa ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba ziara yake nchini humo inaendana na desturi yake ya kila mwaka ya kutembelea nchi za Kiislamu wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa "kufunga kwa mshikamano na kushiriki Iftari."

Wizara ya Mambo ya nje ya Somalia imesema umuhimu wa ziara hiyo ni kufanya mazungumzo ya kisiasa, usalama, maendeleo na kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.