Pata taarifa kuu

Kero la mabomu yaliotegwa ardhini nchini Sudan Kusini

NAIROBI – Dunia hivi leo inaadhimisha siku ya kimataifa ya kuhamasisha uondoaji wa mabomu ya kutegwa ardhini.Nchini Sudan Kusini, watu zaidi ya elfu 5 wameripotiwa kufa kutokana na milipuko ya kutegwa ardhini, huku mamia ya hekari ya ardhi yake ikitajwa kusheheni mabomu ya kutegwa.

Mji mkuu wa Sudani Kusini Juba.
Mji mkuu wa Sudani Kusini Juba. Aguek/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Itta Betty Mogga raia wa Sudan Kusini aliyepata mafunzo kuhusu namna ua kuondoa mabomu ardhini anaelezea hali halisi katika nchi yake.

“Mabomu ya ardhini na vilipuzi ambayo yangali kwenye sehemu ambazo zilikumbwa na mapigano, ni hatari kwa usalama wa watu. Kdri tunavyopigana vita dhidi ya gonjwa hatari la korona, inabidi kuelewa kuwa kuna vitu ambavyo ni hatari jinsi hali ilivyo sasa.“amesema Itta Betty Mogga raia wa Sudan Kusini.
00:22

Itta Betty Mogga raia wa Sudan Kusini

Serikali inakiri kuwa, bado inaendelea kukabiliwa na changamoto kuondoa mabomu hayo kama anavyoeleza Jurkuch Barach Jurkuch, mwenyekiti wa shirika la taifa la Sudan Kusini linalohusika na uondoaji wa mabomu.

“Mabomu haya yalitegwa ardhini wakati wa vita lakini kwa sasa hakuna vita. Hata hivyo inafaa ikumbukwe kuwa mabomu yaliyoko ardhini hayana muda wa kuoza bali yanaweza kuwemo ardhini kwa miaka mingi, ili mradi tu hayachokozwi au kuchokorwa na mtu. “ameeleza Jurkuch Barach Jurkuch, mwenyekiti wa shirika la taifa la Sudan Kusini linalohusika na uondoaji wa mabomu.
00:29

Jurkuch Barach Jurkuch, Kuhusu Mabomu Sudan Kusini

Tangu Sudan Kusini iwe nchi huru julai 2011 zaidi ya mabomu bilioni moja yaliyolenga binadamu, yameharibiwa, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Naye, mkurugenzi wa shirika linalohusika na uondoaji wa mabomu Sudan Kusini, Francis William Ogrady, anasaema kuwa tangu mwaka 2006 zaidi ya mita bilioni moja mraba zimethibitishwa kuwa salama kutokana na kazi ya uondoaji wa mabomu.  Mita milioni 16 mraba zingali haziandolewa mabomu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.