Pata taarifa kuu

Burkina Faso: Utawala wa kijeshi watangaza kusitishwa kwa matangazo ya France 24

NAIROBI – Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso, umetangaza kusitisha matangazo ya kituo cha televisheni cha Ufaransa, France 24, saa chache baada ya kituo hicho kurusha mahojiano na kiongozi wa Al Qaeda ukanda wa Afrika Kaskazini.

Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso, umetangaza kusitisha matangazo ya kituo cha televisheni cha Ufaransa, France 24
Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso, umetangaza kusitisha matangazo ya kituo cha televisheni cha Ufaransa, France 24 © FMM
Matangazo ya kibiashara

Katika tarifa yake, Serikali ya Burkina Faso imesema kitendo cha kituo hicho kurusha mahojiano na kiongozi wa Al Qaeda kwenye êneo hilo, Abu Ubaydah Yusuf al-Annabi, ni wazi kinakiuka sheria za nchi na kimekubali kutumiak kama chombo cha mawasiliano cha kundi hilo.

Jean Emmanuel Oudraogo, ameongeza kwenye tarifa yake kuwa, serikali imesikitishwa na kitendo hicho na kwamba imefikia uamuzi wa kuzuia matangazo ya France 24 nchi nzima.

Katika majibu yake, uongozi wa France 24, umelaani uamuzi wa serikali na kutupilia mbali tuhuma kuwa mahojiano na kiongozi huyo wa Al Qaeda yalikiuka maadili ya kazi yake kama chombo cha habari.

Mwezi Decemba mwaka jana, utawala wa Ouagadogou, ulikifungia kituo cha redio cha RFI ambacho ni kituo mama na France 24, vinavyomilikiwa na France Media Monde, ikikituhumu kituo hicho kwa kutoa habari za vitisho dhidi ya utawala.

RFI na France 24 vyombo vya habari maarufu zaidi kwenye ukanda wa Afrika Magharibi,  matangazo yake pia yamezuiwa kwenye nchi jirani ya Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.