Pata taarifa kuu

Sudan Kusini: WFP yasitisha zoezi la usambazaji wa chakula cha msaada

NAIROBI – Shirika la mpango wa chakula duniani WFP, limesitisha zoezi la usambazaji wa chakula cha msaada kwa watu zaidi ya Milioni 1 katika jimbo la Joglei nchini Sudan Kusini, kwa kile shirika hilo limesema ni kwa sababu za kiusalama.

WFP imesitisha usambazaji wa misaada katika jimbo la Jonglei Sudan Kusini
WFP imesitisha usambazaji wa misaada katika jimbo la Jonglei Sudan Kusini AFP PHOTO / CHARLES LOMODONG
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imethibitishwa na Hellen Magrogty, mwakilishi wa Shirika hilo kwenye jimbo hilo, baada ya kuuawa kwa wafanyakazi wawili wa WFP na zaidi ya 10 kujeruhiwa baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha siku ya Jumtatu.

“Tunatoa wito kwa wakuu wa Sudan kusini kuchukua hatua ya haraka kuimarisha ulinzi kwenye barabara ambazo magari yetu yanapita na pia kuhakikisha kuna usalama wa kutosha kwa wafanyakazi wetu.amesemaHellen Magrogty

00:13

Hellen Magrogty, Mwakilishi wa WFP Jonglei Sudan Kusini

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, nchini humo Farhan Haq, amesema visa vya wafanyakazi wa misaada ya kibinadamau kulengwa na watu wenye silaha, vinaendelea kuongezeka katika eneo hilo.

“Hili ni shambulio la hivi karibuni katika mfululizo wa mashambulizi yanayolenga mashirika ya kutoa misaada na wafanya kazi nchini Sudan Kusini.”ameeleza Farhan Haq

00:10

Farhan Haq, Msemaji wa UN nchini Sudan Kusini

Gordon Kong Bar, Waziri wa baraza la mawaziri jimboni Jonglei anasema serikali katika eneo hilo, inafanya kinachowezekana kuwalinda watoa misaada hao.

 

“Tumepeleka vikosi vyetu vya ulinzi kwenye barabara kudumisha ulinzi Kwa wafanya kazi wa mashirika ya misaada. Yeyote ambaye amewhusika na mashambulizi lazima akabiliwe na sharia. Ikiwa waliohusika watanaswa lazima washitakiwe.amesema Gordon Kong Bar

00:16

Gordon Kong Bar, Waziri wa baraza la mawaziri jimboni Jonglei

Hatua hii imekuja, baada ya Shirika la Umoja Wa mataifa linalohusika na utoaji misaada OCHA kusema watu zaidi ya Milioni tisa, wanahitaji msaada wa chakula nchini Sudan Kusini.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.