Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Raia waandamana katika maeneo tofauti nchini humo

NAIROBI – Upinzani nchini Afrika Kusini umeanzisha maandamano na mikutano ya kisiasa wakati huu usalama ukiimarishwa katika maeneo tofauti katika taifa hilo. 

Members of the Economic Freedom Fighters protest in Cape Town, South Africa, Monday March 20, 2023. The party has called for a nation-wide shutdown and mass demonstrations to press President Cyril Ramaphosa to resign.
Members of the Economic Freedom Fighters protest in Cape Town, South Africa, Monday March 20, 2023. The party has called for a nation-wide shutdown and mass demonstrations to press President Cyril Ramaphosa to resign. AP - Nardus Engelbrecht
Matangazo ya kibiashara

Chama cha upinzani nchini humo kinasema kimechukua hatua hii kama njia moja ya kumshinikiza rais Cyril Ramaphosa kutatua suala la mfumuko wa bei na kukatika kwa umeme kila mara. 

Maelfu ya waandamanaji walikusanyika katika mji mkuu Pretoria wakijiandaa kuandamana hadi kwenye Majengo ya Muungano, makao makuu ya serikali, ambapo polisi na wanajeshi walikuwa wakishika doria. 

Raia wengine walikusanyika katika maeneo mengine ya nchi, kulingana na picha kwenye vyombo vya habari vya ndani na kwenye mitandao ya kijamii. 

Kwa mujibu wa maofisa wa polisi nchini Afrika Kusini karibia waaandamanaji wanane walikamatwa usiku wa kuamkia leo Jumatatu kwa kuhusishwa na ghasia. 

Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF), chama cha tatu kwa ukubwa nchini humo, kimetoa wito wa kufanyika kwa mgomo  na maandamano, na hivyo kuzua hofu ya kurudiwa kwa machafuko ambayo yalisababisha vifo vya miaka miwili iliyopita. 

Shughuli za uchukuzi na biashara zimeripotiwa kuathirika wengi wa wafanyibaishara wakihofia kuharibiwa kwa mali yao na waandamanaji. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.