Pata taarifa kuu

DRC: Matarajio ya wakimbizi wa ndani wakati wa ziara ya ujumbe wa Baraza la Usalama

Hali ya usalama mashariki mwa DRC, itagubika mkutano kati ya Rais wa Kongo Félix Tshisekedi na ujumbe wa Umoja wa Mataifa, katika ziara ya siku tatu nchini humo. Mkuu wa Nchi alikutana Ijumaa Machi 10 na wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na mkuu wa MONUSCOkatika eneo la Umoja wa Afrika huko Kinshasa.

Waasi wa M23 huko Kibumba, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Desemba 23, 2022.
Waasi wa M23 huko Kibumba, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Desemba 23, 2022. AFP - GLODY MURHABAZI
Matangazo ya kibiashara

Rais Félix Tshisekedi, aliwakaribisha katika "Congo, nchi iliyovamiwa", kwa maneno yake, kwa mara nyingine akiishutumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi wa M23. Ikiwa Kinshasa inatarajia kuona vikwazo dhidi ya Kigali, wawakilishi wa Baraza hilo wanasalia kuwa waangalifu.

Moja ya malengo ya ziara yao ni kutathmini hali ya usalama katika mkoa wa Kivu Kaskazini na walithibitisha kuunga mkono Ujumbe wa Umoja wa Mataifa, MONUSCO, "suluhisho bora", kulingana na wao, "kurejesha amani . »

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja  Mataifa wamewasili Jumamosi hii, Machi 11, mjini Goma. Saa chache kabla ya kuwasili kwao, Patient Ligodi, mwaandishi wetu maalum katika eneo hili, alizuru maeneo ya watu waliokimbia makazi yao karibu na Goma.

'M23 inatufanya tuteseke sana'

Bizimana ni mkaazi wa mji wa Rumangabo. Yeye, mke wake na watoto watano walikimbia vurugu na kuishi katika maturubai huko Kanyaruchinya, karibu na mji wa Goma: "M23 inatufanya tuteseke sana. Watu hawa wanatuua kama wanyama. Walitukataza hata kwenda kwenye mashamba yetu ambayo yapo Rumangabo. Ukithubutu kwenda huko watakuua”.

Hafurahii tena maisha ya kambini. Anatumai Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litasikia kilio chake: “Naomba watusaidie. Tunataka kwenda nyumbani. Maisha hapa ni magumu sana. Tunateseka sana! ".

'Kwa sasa hali ni ngumu'

Upande wapili wa jiji, Josée alikimbia Saké, jiji lililo umbali wa chini ya kilomita 30 kutoka mji wa Goma. Yeye na watoto wake walipata hifadhi siku ya Ijumaa asubuhi katika shule katika eneo la Lac Vert. Pia anatumai kuwa Baraza la Usalama la Umoja a Mataifa litahusika zaidi katika kukomesha kusonga mbele kwa M23: "Tulikimbia tuliposikia milipuko ya mabomu katikati mwa Saké. Tumeamua kukimbia, sisi tulio na watoto. Kwa sasa hali ni ngumu.”

Hadi Ijumaa jioni, wanawake, watoto na wazee walikaribia mji wa Goma, wakiukimbia mji wa Saké.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.