Pata taarifa kuu

Wahamiaji 14 wakufa maji katika pwani ya Tunisia

Wahamiaji 14 kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara walikufa maji na wengine hamsini na wanne waliokolewa baada ya kuzama kwa boti iliyokuwa imewabeba kutoka pwani ya Tunisia, walinzi wa pwani wametangaza Alhamisi.

Wahamiaji wakiokolewa kwenye pwani ya Sfax walipokuwa wakijaribu kuingia Italia mnamo Oktoba 4, 2022.
Wahamiaji wakiokolewa kwenye pwani ya Sfax walipokuwa wakijaribu kuingia Italia mnamo Oktoba 4, 2022. AFP - FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Boti iliyokuwa imewabeba wahamiaji hao ilizama kwenye eneo la Sfax (katikati-mashariki) usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi na walinzi wa pwani "waliokoa miili kumi na minne ya wahamiaji na kuwaokoa wahamiaji wengine 54 wakiwa hai", amesema msemaji wa Walinzi wa Pwani ya Tunisia kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Ajali hii ya boti inakuja wakati ambapo wahamiaji wengi kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wanataka kuondoka Tunisia baada ya matamshi ya Rais wa Tunisia Kais Saied dhidi ya uhamiaji haramu.

Mnamo Februari 21, Bw. Saied alisema kuwa kuwepo nchini Tunisia kwa "makundi" ya wahamiaji haramu kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara ni chanzo cha "vurugu na uhalifu" na ni sehemu ya "biashara ya uhalifu" yenye lengo la "kubadilisha muundo wa idadi ya watu." "nchini.

Baada ya hotuba hii, iliyolaaniwa na mashirika yasiyo ya kiserikali kuita kama "ya kibaguzi na chuki", raia wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara waliripoti kuongezeka kwa mashambulizi dhidi yao na kukimbizwa na makumi ya watu kwenye balozi zao ili kurejeshwa makwao.

Kulingana na takwimu rasmi, Tunisia ina zaidi ya raia 21,000 kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, wengi wao wakiwa hawana vibali vinavyowaruhusu kuishi nchini humo, ambayo ni chini ya 0.2% ya jumla ya watu karibu milioni 12.

Tunisia, nchi ya Afrika Kaskazini yenye sehemu fulani za ufuo ulio chini ya kilomita 150 kutoka kisiwa cha Italia cha Lampedusa, mara kwa mara hurekodi majaribio ya kuwaacha wahamiaji kwenda Italia. Kwa mujibu wa takwimu rasmi za Italia, zaidi ya wahamiaji 32,000 wakiwemo 18,000 wa Tunisia waliwasili nchini Italia kinyume cha sheria kutoka Tunisia mwaka 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.