Pata taarifa kuu

Uchumi wa Afrika Kusini washuka

NAIROBI – Uchumi wa Afrika Kusini, umeshuka kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita, wakati huu, nchi hiyo iliyowahi kuongoza kwa uchumi mkubwa barani Afrika, ikiendelea kukabiliwa na kukatika kwa umeme.

 Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa AP
Matangazo ya kibiashara

Takwimu zinaonesha kuwa, uchumi wa nchi hiyo yenye utajiri wa viwanda barani Afrika, ulishuka kwa asilimia 1.3 kwa kipindi hicho cha miezi mitatu mwaka uliopita, wakati huu watalaam wakisema uchumi huo unatarajiwa kukua kwa asilimia 0.3 mwaka huu.

Idara inayohusika na takwimu nchini humo inasema hali hiyo ilichangiwa na janga la uviko 19, baada ya hapo awali, uchumi kuonekana kukua kwa asilimia 1.6 kati ya mwezi Julai na Septemba.

Uchumi wa nchi hiyo, ulitikiswa kutokana na janga hilo ambalo pia lilisababisha, idadi kubwa ya watu kupoteza ajira.

Haya yanajiri katika kipindi ambacho nchi hiyo ikakabiliwa na uhaba wa umeme, baada ya kampuni ya kuzalisha bidhaa hiyo kueleza kuwa, mitambo yake ilikuwa imeharibika.

Rais Cyril Ramaphosa, amemteua Waziri mpya wa umeme Kgosientsho Ramokgopa, kusaidia kuimarisha tena sekta ya nishati nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.