Pata taarifa kuu

DRC: WHO yasaidia waathiriwa 104 wa unyanyasaji wa kijinsia mikononi mwa mashirika ya misaada

Takriban waathiriwa 100 wa unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na wafanyakazi wa misaada nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamepokea msaada unaofadhiliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), WHO ilitangaza Jumanne, wakati shirika hili la Umoja wa Mataifa limekuwa likikosolewa kwa kuchelewa kuchukuwa hatua.

Huko Kananga, MSF inatibu zaidi ya wanawake 15 waliobakwa kwa siku.
Huko Kananga, MSF inatibu zaidi ya wanawake 15 waliobakwa kwa siku. © Sonia Rolley/RFI
Matangazo ya kibiashara

Kati ya waathiriwa 115 wa unyanyasaji wa kijinsia ukatili uliofanywa na wafanyakazi wa misaada wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika miaka ya 2018-2020 waliotambuliwa hadi sasa, 104 wamekubali kusaidiwa, amesema Dk Eugène Kongnyuy, mwakilishi Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) nchini DRC, wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

DRC: Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wawatelekeza wanawake wajawazito na watoto wasio na baba

Shirikalinalopiga vita unyanyasaji wa kijinsia limepewa jukumu na WHO kuwatafuta waathiriwa, ambao wako katika maingira magumu, na kuwapa usaidizi, iwe katika kiwango cha matibabu, kisaikolojia au kifedha, amebaini Daktari Gaya Gamhewage anayehusika na masuala ya kuzuia na matibabu ya unyanyasaji wa kijinsia ndani ya WHO. Hivyo, UNFPA ilibidi kutafuta njia za kutoa msaada wa muda mrefu kwa watoto 17 waliozaliwa kutokana na unyanyasaji huu wa kijinsia.

"Inabidi tuwatunze watoto katika suala la elimu na lishe. Na kisha tufanye vipimo vya DNA ili kutambua baba zao. Hadi tutakapomjua baba, tunapaswa kujua jinsi ya kuendelea kumtunza mtoto." , amesema Dk Kongnyuy.

WHO, ambayo ina hazina maalum iliyojaliwa dola milioni 2, imetoa 350,000 kwa wakati huu kufadhili ubia nchini DRC. Inalipa wahasiriwa wote, hata ikiwa ni theluthi moja tu wamedhulumiwa na wafanyikazi wake au wakandarasi wadogo.

Mwishoni mwa mwaka wa 2021, ripoti huru ilionyesha kwamba wafanyakazi 21 wa WHO walikuwa miongoni mwa wafanyakazi 83 wa kibinadamu wanaoshutumiwa kwa unyanyasaji wa kingono na unyanyasaji dhidi ya makumi ya watu nchini DRC wakati wa janga hili la Ebola, katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri (mashariki).

Mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa pia yalihusika, lakini tahadhari ilikuwa imelenga WHO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.