Pata taarifa kuu

Macron kubadilisha sera kuhusu wanajeshi wake barani Afrika

NAIROBI – Hotuba ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alioitoa jana Kabla ya kuanza, ziara yake katika bara la Afrika Jumatano March Mosi ambayo itampeleka Gabon, Angola, Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imepokelewa kwa hisia mseto na watu kutoka katika mataifa mbalimbali Barani Afrika. 

 Emmanuel Macron,Rais wa Ufaransa
Emmanuel Macron,Rais wa Ufaransa REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba hiyo Emmanuel Macron amesema Ufaransa inafungua ukurasa mpya ambapo swala la usalama sio kipaombele cha mkakati wake, na kwamba hataki kushiriki katika mashindano ya nguvu kwa kupeleka vikosi vya kijeshi barani Afrika, na kwamba mfumo wa uwepo wa vikosi vya Ufaransa barani Afrika hautakuwa kama ilivyokuwa hapo awali.

“Sehemu ambayo kutakuwa na vikosi zaidi ya wanajeshi mia moja au zaidi ya wanajeshi Elfu moja wa Ufaransa tutapunguza kiasi cha wanajeshi wetu ambapo vituo hivyo havitafungwa.”amesema rais Emmanuel Macron.

00:19

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu Wanajeshi wake Afrika

Aidha kuhusu swala la mzozo mashariki mwa DRC, Emmanuel Macron amesema Vita vya waasi wa M23 mashariki mwa DRC vinairudishi miaka kumi nyuma.

“Mashambulio ya waasi wa M23 walio chini ya vikwazo vya baraza la usalama wa Umoja na mataifa ni vita vinavyoturejesha miaka 10 nyuma na vina madhara makubwa kwa wanachi.” amesisitiza rais Emmanuel Macron

00:23

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu waasi wa M23 nchini DRC

Upande wake waziri wa mambo ya nje wa DRC Christophe Lutundula amesema msimamo wa Ufaransa dhidi ya Rwanda lazima uwe wazi.

“Nadhani kwamba msimamo wa Ufaransa dhidi ya Rwanda lazima uwe wazi, Ufaransa imeitaka Rwanda kusitisha uungwaji wake mkono wa M23.”amesema Christophe Lutundula.

00:20

Christophe Lutundula, Waziri wa Mambo ya nje wa DRC

Mashirika ya kirai Barani Afrika kama vile Balai Citoyen la huko Burkinafaso limesema lazima Ufaransa ielewe kwamba upepo umebadilika. Ziara hiyo ya Emmanuel Macron barani Afrika itakuwa ni ya 18 na ya pili Afrika ya kati

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.