Pata taarifa kuu

Matokeo na maamuzi ya mkutano wa 36 wa Umoja wa Afrika

Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika ulimalizika Jumapili Februari 19 huko Addis Ababa, Ethiopia. Wahusika wakuu walipitisha makumi ya maamuzi, matamko, maazimio na hoja nyinginezo ambazo zilikuwa zimejadiliwa vikali ndani ya Halmashauri Kuu ya umoja huo. Azali Assoumani, rais wa Comoro, alichukua nafasi ya mkuu wa AU kwa mwaka mmoja.

Viongozi kadhaa wa Afrika, akiwemo Rais anayemaliza muda wake wa Umoja wa Afrika Macky Sall wa Senegal (wa pili kulia), wakiwasili katika makao makuu ya umoja huo kwa siku ya pili ya mkutano wa 36.
Viongozi kadhaa wa Afrika, akiwemo Rais anayemaliza muda wake wa Umoja wa Afrika Macky Sall wa Senegal (wa pili kulia), wakiwasili katika makao makuu ya umoja huo kwa siku ya pili ya mkutano wa 36. AFP - TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Nakala kadhaa zilizopitishwa Jumapili Februari 19 ni pamoja na uamuzi wa ripoti ya Rais wa Rwanda Paul Kagame juu ya mageuzi ya kitaasisi ya Umoja wa Afrika baada ya Rais wa Senegal anayemaliza muda wake, Macky Sall, kwa kupitisha azimio ambalo linarejea kila mwaka kuhusu kuondolewa kwa kizuizi ambacho Marekani imeiwekea Cuba kwa miongo kadhaa.

Hoja ambazo hapakuwa na maafikiano katika ngazi ya Mawaziri ziliachwa kwa uamuzi wa Wakuu wa Nchi, lakini baadhi ya hoja hizo bado hazijatatuliwa. Hadhi ya mwangalizi iliyopewa Israeli na kusimamishwa kwa mwaka mmoja kusubiri ripoti ya kamati ya muda ambayo haijakutana hadi sasa. Kwa hiyo Wakuu wa Nchi wameamua kusubiri hitimisho lake. "Ni njia yao ya kuliondoa tatizo ambalo linawagawanya", afisa wa nagazi ya juu katika Umoja wa Afrika amebaini.

Nyingi za hati hizi ni za matamanio. "Wanarudi kila mwaka, karibu katika hali kama hiyo," kinaongeza chanzo kimoja. Isipokuwa ile "inayowahusu zaidi," amesema, akirejelea ripoti ya Baraza la Amani na Usalama kuhusu migogoro mbalimbali inayotikisa bara hilo.

Kuandaa mkutano wa maridhiano nchini Libya, kuimarishwa kwa vikwazo dhidi ya Mali, Burkina Faso na Guinea, uamuzi uliochukuliwa na ECOWAS, au hata kuidhinisha maamuzi ya mkutano mdogo wa Mashariki mwa DRC... Lakini hiyo haimaanishi kwamba migogoro yote hii itatatuliwa kwa wakati mmoja, afisa huyo wa Umoja wa Afrika ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.