Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Guinea: Mapigano na ukandamizaji wa wito wa kuandamana katika vitongoji vya Conakry

Makabiliano yamezuka kati ya vijana na vikosi vya usalama vya Guinea siku ya Alhamisi katika vitongoji vya Conakry ambako upinzani uliitisha maandamano licha ya utawala wa kijeshi kupiga marufuku mikusanyiko yoyote, waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP wamebainisha.

Guinea imetawaliwa tangu Septemba 2021 na jeshi ambalo lilichukua mamlaka kwa nguvu mnamo Septemba 5, 2021 katika mojawapo ya maeneo mbalimbali ambayo Afrika Magharibi imepitia kwa miaka miwili. Utawala wa kijeshi umepiga marufuku maandamano yoyote tangu 2022. Pia umtangaza kuvunjwa kwa FNDC.
Guinea imetawaliwa tangu Septemba 2021 na jeshi ambalo lilichukua mamlaka kwa nguvu mnamo Septemba 5, 2021 katika mojawapo ya maeneo mbalimbali ambayo Afrika Magharibi imepitia kwa miaka miwili. Utawala wa kijeshi umepiga marufuku maandamano yoyote tangu 2022. Pia umtangaza kuvunjwa kwa FNDC. AFP - CELLOU BINANI
Matangazo ya kibiashara

Maeneo kadhaa kando ya barabara ya Le Prince inayoingia katika kitongoji cha mji wa Conakry yameshuhudia makabiliano ya mara kwa mara kati ya vikundi vinavyotembea vikirusha mawe na kuweka vizuizi barabarani, na askari na maafisa wa polisi wakijaribu kuwatawanya kwa mabomu ya machozi. Milio ya risasi imesikika.

Mapigano yaliripotiwa mapema Jumatano jioni. Vuguvugu linalodai kutetea Katiba (FNDC), muungano makundi yanayotetea haki, umebaini  katika taarifa kwa vyombo vya habari mapema Alhamisi kwamba watu sita walipigwa risasi na kujeruhiwa, ambapo mmoja wao, kulingana na muungano huo, yuko katika hali mbaya.

FNDC imehakikisha kwamba mamlaka iliita vitengo vya jeshi kuja kusaidia wenzao. Matumizi ya jeshi ni "hali ya kutia wasiwasi kwa vile hatuelewi ni nini kinaweza kuhalalisha uamuzi kama huo katika hatua hii", amesema Alseny Sall msemaji wa vuguvugu linalodai kutetea haki za Binadamu lnchini Guinea.

FNDC ilikuwa imeitisha maandamano ya kutaka viongozi wake watatu waliokamatwa na wafungwa wengine wote waachiliwe kwa sababu zinazoaminika kuwa za kisiasa, pamoja na kurejea kwa haraka kwa raia madarakani.

Guinea imetawaliwa tangu Septemba 2021 na jeshi ambalo lilichukua mamlaka kwa nguvu mnamo Septemba 5, 2021 katika mojawapo ya maeneo mbalimbali ambayo Afrika Magharibi imepitia kwa miaka miwili. Utawala wa kijeshi umepiga marufuku maandamano yoyote tangu 2022. Pia umtangaza kuvunjwa kwa FNDC.

Wanajeshi wameahidi kutoa nafasi kwa raia waliochaguliwa baada ya kipindi ambacho wanasema wanataka kufanya mageuzi makubwa. Wanajeshi hao wakiongozwa na Kanali Mamady Doumbouya walikubali chini ya shinikizo kutoka kwa jumuiya ya mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS, kuweka kikomo kipindi hiki cha mpito hadi miaka miwili kuanzia Januari 2023.

Upinzani unashutumu serikali kwa kunyang'anya mamlaka na kunyamazisha sauti zozote zinazopingana kupitia kukamatwa kwa viongozi wa kisiasa au mashirika ya kiraia, na maswali ya mahakama. Vyama vikuu vinakataa mazungumzo na utawala wa kijeshi juu ya yaliyomo katika kile kinachoitwa kipindi cha mpito chini ya masharti yaliyowekwa na mamlaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.