Pata taarifa kuu

Wanajeshi wa Somaliland washambuliwa na watu wenye silaha

Wanajeshi wa jimbo la Somaliland nchini Somalia, wameshambuliwa na watu wenye silaha, licha ya kuwepo kwa maelewano ya kusitisha mapigano makali ambayo yamekuwa yakiendelea wiki hii.

Un soldat du territoire séparatiste somalien du Somaliland monte la garde lors du défilé du jour de l'indépendance dans la capitale, Hargeisa, le 18 mai 2016.
Un soldat du territoire séparatiste somalien du Somaliland monte la garde lors du défilé du jour de l'indépendance dans la capitale, Hargeisa, le 18 mai 2016. AFP - MOHAMED ABDIWAHAB
Matangazo ya kibiashara

Mashambulio haya yamekuja baada ya Abdiqani Mahamoud Ateye, Waziri wa Ulinzi katika jimbo hilo kutangaza makubaliano ya kuacha makabiliano bila masharti yoyote.

Licha ya shambulio hilo, Waziri huyo amesema jeshi la Somaliland lilifanikiwa kujilinda na hali ya tahadhari inashuhudiwa katika kambi yao ya Las Anod.

Wiki hii watu 20 waliuawa baada ya mapigano kati ya wanajeshi wa jimbo hilo na kundi lenye silaha katika mji unaowaniwa wa Las Anod, unaopambaniwa na uongozi wa jimbo hilo na jimbo lingine la Puntland.

Somaliland,ilijitangazia uhuru wake tangu 1991 kutoka uongozi wa Mogadishu, lakini haijawahi kutambuliwa kimataifa, licha ya kuendelea kushuhuhudia uthabiti hasa wa kisiasa na usalama kwa kipindi kirefu  nchini humo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.