Pata taarifa kuu

Rapa kutoka Afrika Kusini Kiernan Jarryd Forbes AKA auawa kwa kupigwa risase

Taarifa za mauaji ya mwanamuziki rapa kutoka nchini Afrika Kusini Kiernan Jarryd Forbes maarufu AKA zilianza kusambaa mitandaoni kuanzia alfajiri kabla ya kuthibitishwa na familia yake ambayo imebaini maskitiko yake kufuatia kifo cha kijana wao alieuliwa katika mazingira tatanishi.

Kiernan Jarryd Forbes
Kiernan Jarryd Forbes © AKA facebook
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zinasema tarehe 10 Februari 2023 majira ya saa nne usiku sawa na saa tatu majira ya Afrika Mashariki, Forbes alipigwa risasi na kuuawa katika eneo maarufu la starehe za  usiku kwenye Barabara ya Florida huko Durban wakati akijiandaa kuelekea kwenye muendelezo wa sherehe ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake.

Kulingana na shahidi katika eneo la tukio, Forbes alipigwa risasi akiwa amesimama kwenye lami wakati milio ya risasi ilisikika muda mfupi baada ya saa nne usiku wa kumakia Jumamosi.

AKA na rafiki yake Tebello 'Tibz
AKA na rafiki yake Tebello 'Tibz © AKA facebook

 

Rafiki wa AKA Tebello 'Tibz' Motsoane alipigwa risasi na rapper huyo. Tibz alikuwa na bidii sana katika kuchagiza taaluma ya AKA siku za mwanzo na walibaki kuwa watu wa karibu tangu wakati huo.

Tukio hilo lilitokea dakika chache baada ya kula chakula cha jioni kwenye mgahawa wa Wish OnFlorida.

Alipangiwa kutumbuiza usiku uleule aliopigwa risasi kwenye klabu ya Yugo night huko Durban na ilibidi onyesho lisitishwe.

Familia yake Tony na Lynn Forbes ambao ni Wazazi wa Rapper wamethibitisha kupitia taarifa walioitoa

 

Familia yathibitisha kifo cha AKA
Familia yathibitisha kifo cha AKA © AKA facebook

 

“Kwa masikitiko makubwa tunathibitisha kifo cha Mpendwa Mtoto wetu ambaye amefariki kifo cha kusikitisha jioni ya Feb 10,2023, tunasubiri taarifa zaidi kutoka Polisi wa Durban”

“Kwetu Kierman alikuwa Mtoto wetu, Kaka, Mjukuu, Binamu na Rafiki na zaidi Baba wa Mtoto wake Mpendwa wa kike Kairo, kwa Watu wengine wengi alikuwa AKA, SUPAMEGA, BHOVA na majina mengine mengine ambayo Mashabiki zake walimuita”

AKA aliwahi kushirikiana na mwanamuziki Diamond Plutnumz katika wimbo "Make me sing". Diamond Platnumz ameandika kupitia mitandao yake ya kijamii akibaini maskitiko yake kufuatia kifo hicho. Mbali na Diamond Platnumz kutoka nchini Tanzania, mwanamuziki Joh Makini ambae aliwa kumshirikisha katika wimbo wake Don't bodher ametuma pia salam za rambirambi kwa familia.

Jina lake halisi ni Kiernan Jarryd Forbes aliezaliwa  Januari 28 mwaka 1988 anajulikana kama AKA, alikuwa rapper wa Afrika Kusini. Alizaliwa na kukulia Cape Town, Forbes alipata kutambuliwa baada ya kuachia wimbo wake "Victory Lap" kutoka katika albamu yake ya kwanza ya studio, Altar Ego (2010).

Forbes iliendelea na mafanikio yake kwa kutoa albamu za studio ambazo ni pamoja na Levels (2014), Touch My Blood (2018), Bhovamania (2020), na albamu ya ushirikiano na Anatii, iliyoitwa Be Careful What You Wish For (2017).

Kuhusu Maisha yake binafsi

Forbes alianzisha mahusiano na mtayarishaji ama DJ Zinhle mwishoni mwa mwaka 2014. Baada ya kupokea tuzo kadhaa za Tuzo za Hip Hop za Afrika Kusini, Zinhle alidokeza uhusiano wao kwa kutuma ujumbe kwenye Twitter "Hongera kwa mshindi wangu, Wawili hao walifaanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike anayeitwa Kairo Olwethu Forbes, aliyezaliwa mwaka wa 2015.

Agosti mwaka 2015, Forbes na Zinhle walitengana baada ya taarifa kuwa Forbes alidaiwa kumlaghai Zinhle na kutoka na mtangazaji wa televisheni Bonang Matheba. Awali wawili hao walikanusha madai hayo, Lakini mwaka 2016 walithibitisha kutoka kimapenzi. Forbes na Matheba walitengana Desemba 2017. Hata hivyo, Forbes na Zinhle walirudi pamoja mwishoni mwa 2018, ingawa baadaye mwaka wa 2019 waliachana tena.

Tarehe 21 Februari 2021, Forbes alichapisha picha kwenye Instagram ikitangaza uchumba wake na mpenzi wake Nelli Tembe. Tarehe 11 Aprili 2021, Tembe alifariki baada ya kuanguka kutoka hoteli moja mjini Cape Town.

Kufuatia kifo cha Tembe, ziliibuka taarifa kuwa Forbes amekuwa akitumia dawa za kulevya. Taarifa ambazo hata hivyo alizikanusha licha ya kuonekana kwa ushahidi kadhaa.

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.