Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Mkuu wa kitengo cha haki za binadamu cha MINUSMA afukuzwa nchini Mali

Kufukuzwa kwa kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa kunakuja baada ya ukosoaji mkubwa wa Aminata Dicko katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mnamo Januari 27. Pia hatua ya kufukuzwa kwa Mkuu wa kitengo cha haki za binadamu cha MINUSMA inafuata ile ya mwakilishi wa ECOWAS na ile ya balozi wa Ufaransa, baada ya kuondoka kwa Barkhane.

Guillaume Ngefa-Atondoko Andali (hapa ilikuwa mnamo mwaka 2011) apewa saa 48 kuwa ameondoka nchini Mali.
Guillaume Ngefa-Atondoko Andali (hapa ilikuwa mnamo mwaka 2011) apewa saa 48 kuwa ameondoka nchini Mali. AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Saa 48 ndio muda wa mwisho uliyotangazwa rasmi na msemaji wa serikali ya Mali katika taarifa kwa vyombo vya habari kwenye televisheni kwa Guillaume Ngefa-Atondoko Andali kuondoka nchini Mali. Sababu iliyotolewa: upendeleo unaodhaniwa wa mkuu wa kitengo cha haki za binadamu cha MINUSMA. Mamlaka ya mpito inamtuhumu kwa kuweka mbele Aminata Dicko kama mwakilishi wa mashirika ya kiraia katika Baraza la Usalama la Umoja w Mataifa siku tisa zilizopita. Naibu kiongozi wa shirika la KISAL hakusita kukemea hali ya usalama nchini humo na kuhusisha washirika wapya kutoka Urusi wa jeshi la kitaifa katika ukiukaji mkubwa ... madai ambayo yaliaghadhabisha Bamako.

Umoja wa Mataifa umeiambia RFI "kusikitishwa na uamuzi wa serikali ya Mali", huku ukibaini kwamba MINUSMA "itaendeleza utekelezaji wa mamlaka yake, ikiwa ni pamoja na kuhusu haki za binadamu". Umoja wa Mataifa pia umetuthibitishia kwamba haikuwa mkurugenzi wa kitengo cha haki za binadamu aliyemwalika Aminata Dicko, kama inavyodai mamlaka ya Mali, bali ni Japani, ambayo iliongoza Baraza hilo mwezi Januari. Kwa vyovyote vile, Guillaume Ngefa alikuwa analengwa na mamlaka ya Mali kwa muda mrefu. Aliponea kufukuzwa miezi sita iliyopita.

Raia huyo kutoka Congo aneongoza kitengo cha haki za binadamu na ulinzi cha MINUSMA tangu kuundwa kwake mwaka 2013. Kitengo hiki kina jukumu la kuchunguza uhalifu uliofanywa na wahusika wote waliopo nchini Mali: pia kitengo hiki kiliandika madai ya unyanyasaji wa Barkhane huko Bounti mwaka 2022. Na kilidai bila mafanikio kufika katika maeneo yanayodhaniwa kuwa ya kijeshi kulikofanyiwa mauaji, tukio la mwisho liliripotiwa katika kijiji cha Moura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.