Pata taarifa kuu
DRC - USALAMA

DRC: Raia wazungumzia kikao cha wakuu wa nchi za EAC, nchini Burundi

Raia kwenye eneo la mashariki mwa DRC, wametoa hisia mseto baada ya kikao cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kilichofanyika mwishoni mwa juma lililopita nchini Burundi, ambapo wametaka kusitishwa kwa mapigano, na makundi ya waasi kuondoka katika maeneo wanayoshikilia.

Kikao cha wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Bujumbura, Burundi, Februari, 4, 2023
Kikao cha wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Bujumbura, Burundi, Februari, 4, 2023 © EAC
Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya kiraia kwa upande wao yamewataka raia kuwa na matumaini kwa jeshi la nchi, huku wakiwataka wanajeshi wa jumuia ya Afrika mashariki kuondoka nchini DRC, kama anavyoeleza Jeacques Sinzahera kutoka shirika la raia Amka nchini Congo.

 “Tunalisihi jeshi letu la Congo FARDC kupambana na makundi hayo ya ugaidi na raia wote wawe nyuma ya jeshi letu, kwa kusema usalama utatoka kwetu sisi.”amesema Jeacques Sinzahera.

Tangu Jumapili raia waliweka vizuizi barabarani jijini Goma, huku waandamanaji wakipinga mchango wa EAC ambao wanasema hauna manufaa.

“M23 kwanza waende pamoja na maaskari hao wa kigeni waliokuja, tuna wanajeshi wetu wanaofaa, tutaandamana tu kupinga wanajeshi wanaotoka nchi za kigeni.”ameeleza raia wa Goma.

Mkoani Kivu kaskazini Serikali ya Congo haijatoa tamko lolote dhidi ya madai hayo ya raia, wakati huu M23 ikiendelea kushtumiwa kuzidisha mapigano kwenye uwanja wa mapigano wilayani Rutshuru Na Masisi.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.