Pata taarifa kuu
DRC - USALAMA

DRC: Maandamano zaidi mjini Goma kupinga uwepo wa vikosi vya EAC na MONUSCO

Mjini Goma kumekuwa na maandamano ya raia, dhidi ya kikosi cha pamoja cha Jumuiya ya Afrika Mashariki na MONUSCO kwa madai ya kushindwa kukabiliana na waasi wa M23, mkoani Kivu Kaskazini, wanaoendelea kupambana na wanajeshi wa FARDC.

Raia wameendelea kushiriki maandamano mjini Goma, kupinga uwepo wa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini DRC.
Raia wameendelea kushiriki maandamano mjini Goma, kupinga uwepo wa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini DRC. AFP - GUERCHOM NDEBO
Matangazo ya kibiashara

Maandamano haya ya mapema hivi leo, yamekwamisha shughuli mbalimbali huku shule, maduka, benki na vituo vya gesi vikikosa kufanya kazi, huku ripoti zikisema waandamanaji hao walivamia na kubomoa makanisa mawili, yenye jamii ya Banyamulenge mjini Goma. 

Tunapinga EAC kuwa nchini mwetu kama wachunguzi tu, tumegundua EAC na MONUSCO wote wamezembea na hivyo tunataka waondoke, sisi tuko nyuma ya jeshi letu” amesema raia wa Goma.

Waandamanaji waliitikia wito uliotolewa na mashirika ya kiraia, na huyu hapa ni Jules Makeusa, mwanaharakati kutoka MNLC, jijini Goma.

Watu tumewataka wasifanye kazi zao, ili tuonyeshe hasira yetu dhidi ya kuvamiwa na Rwanda, dunia inatazama na haifanyi kitu.” amesema Jules Makeusa.

Licha ya hayo shirika kuu la raia mkoani Kivu Kaskazini halikuunga mkono maandamano haya,  Vicar Hangi Batundi ni mtalaamu wa shirika hilo.

Mji wa Goma uko hatarini na hakungepaswa kuandaliwa maandamano kama haya, lakini hatuwezi kuwazuia raia kuonyesha hasira yao.” amesema Batundi

Juhudi utawala wa eneo hilo na polisi kutaka kukutana na waandamanaji ili kupata mwafaka hazikufua dafu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.