Pata taarifa kuu
RWANDA- USALAMA

Rwanda: Wito umetolewa wa kufanyika uchunguzi huru kuhusu kifo cha John Williams

Mashirika kadhaa ya kutetea haki za binadamu pamoja na vyombo vya habari, wameitaka nchi ya Rwanda kufanya uchunguzi huru na wakina kuhusu mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari mashuhuri nchini humo na mkosoaji wa Serikali.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Rwanda yanataka uchunguzi huru kuabini kifo cha John Williams Ntwali
Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Rwanda yanataka uchunguzi huru kuabini kifo cha John Williams Ntwali Human Rights Watch
Matangazo ya kibiashara

John Williams Ntwali, aliyekuwa mhariri wa jarida la the Chronicles, aliuawa Januari 18 mwaka huu wakati gari lililokuwa kwenye mwendo kuigonga pikipiki aliyokuwa akiitumia.

Ntwali ambaye kabla ya kifo chake, alishakamatwa mara kadhaa na Serikali, anamiliki pia televisheni ya Pax na chaneli ya Youtube, ambazo zilijipambanua kuwa huru na kufanya habari za kina.

Kwa mujibu wa taarifa ya mashirika hayo zaidi ya 90, yanataka Kigali iruhusu uchunguzi huru na wahaki ambao utahusisha wataalamu wa kimataifa, viongozi wakiitaka jumuiya ya kimataifa kuipa shinikizo Rwanda.

Ripoti mbalimbali zinaiweka Rwanda katika nafasi ya 136 duniani kati ya nchi 180 ambazo zinaminya uhuru wa vyombo vya habari na wakosoaji wa serikali ya rais Paul Kagame, ambapo baadhi wamefungwa na wengine kutoweka.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.