Pata taarifa kuu
DRC: ZIARA YA PAPA FRANCIS

Papa Francis yuko nchini DRC kwa ziara ya siku tatu

Kiongozi wa kanisa katoliki dunia Papa Francis, amewasili jijini Kinshasa nchini DRC, ambapo amekutana na rais Felix Tshisekedi, huku akitarajiwa kuzungumza na viongozi wa mashirika ya kiraia na wanadiplomasia.

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis yuko nchini DRC kwa ziara ya siku tatu
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis yuko nchini DRC kwa ziara ya siku tatu REUTERS - LUC GNAGO
Matangazo ya kibiashara

Mwenzangu Carol Korir, amezungumza na Askofu Philip Anyolo, kutoka Dayosis ya Nairobi, kuhusu ziara hii ya Papa Francis.

“Ni baraka nyingi kwa bara la Afrika haswa kwa nchi ya DRC na Sudani kusini ambako kuna mambo mengi ya vita.”amesema Askofu Philip Anyolo

Idadi kubwa ya raia wa DRC ni wahumini wa kanisa Katoliki na wana imani  kuwa ziara ya Papa kwa sehemu kubwa itasaidia katika upatikanaji wa amani eneo la mashariki.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.