Pata taarifa kuu
DRC- VATICAN- ZIARA

DRC: Wakaazi wanamsubiri Papa Francis Jumanne wiki hii

Wakati kiongozi wa kanisa katoliki Duniani Papa Francis akisubiriwa kuwasili hapo kesho jijini Kinshasa, wananchi wa jiji hilo wamebaini furaha yao kumpokea kiongozi huyo ambaye anawasili katika kipindi ambacho DRC inapitia machafuko eneo la mashariki.

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis REUTERS - YARA NARDI
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Kanisa Katoliki katika jimbo la Uvira Askofu Sebastien Muyengo amesema inasikitisha sana kuona swala la kumuuwa mtu limekuwa la kawaida sana mashariki mwa nchi hiyo.

“Tunachoshuhudia mashariki mwa nchi binafsi na shindwa kuelewa watu wanauana kirahisi tu huku ni kupotoka kwa ulimwengu”amesema Sebastien Muyengo.

Rais wa Sudan Kusini, naye amewataka raia wa taifa hilo kudumisha amani wakati wa ziara wa kiongozi wa kanisa katoliki nchini humo, Papa Francis ijumaa hii.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.