Pata taarifa kuu
DRC: ZIARA YA PAPA FRANCIS

DRC: Siku ya Jumatano itakuwa ni mapumziko kwenye jiji la Kinshasa

Serikali ya DRC, imesema siku ya Jumatano itakuwa ni mapumziko kwenye jiji la Kinshasa, ili kutoa nafasi kwa waumini kuhudhuria misa itakayoongozwa na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, ambaye anaanza ziara hapo kesho.

Papa Francis, Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani
Papa Francis, Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani via REUTERS - VATICAN MEDIA
Matangazo ya kibiashara

Ziara yake inakuja wakati huu ambao viongozi wa dini wakitoa wito wa amani na utulivu mashariki mwa nchi hiyo, ambako kunashuhudiwa mapigano kati ya makundi yenye silaha na vikosi vya Serikali.

Kadinali Fridolin Ambongo, ni askofu mkuu wa kanisa katoliki nchini DRC.

“Kwanza ni katika muktadha wa mizozo ndio zaira hii inafanyika raia wa Congo wameteseka kwa miongo kadhaa haswa umaskini huu wakukosewa kila kitu.”ameeleza Fridolin Ambongo.

Papa Francis, anatarajiwa kutumia ziara yake nchini DRC kuhamasisha amani na maridhiano

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.