Pata taarifa kuu
DRC- WHO- AFYA

DRC: Kampeni ya uchomaji Chanjo dhidi ya kipindupindu kwa watoto yaanza

Shirika la afya duniani limeanza kampeni ya miezi sita, kutoa chanjo ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu kwa watoto wenye umri wa mwaka mmoja na kuendelea lakini pia watu wazima katika kambi ya wakimbizi ya Kanyaruchinya, inayotoa makaazi kwa watu waliokimbia vita kati ya waasi wa M 23 na jeshi la DRC jimboni Kivu Kaskazini.

Kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya kipindupindu katika kambi  ya wakimbizi ya Kanyaruchinya  DRC
Kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya kipindupindu katika kambi ya wakimbizi ya Kanyaruchinya DRC © rfi
Matangazo ya kibiashara

Hii inakuja baada ya kuwepo kwa maambukizi karibu Elfu nne, na vifo vya watu 16 kutokana na ugonjwa huo, katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita.

Daktari Bruno Ngenze, ni Mkuu wa WHO katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri.

“Tulipata dozi 364,150 na tuna lengo la kufiikia watu karibia 364,137 ambao watachanjwa kwa dozi moja”. amesema Dkt Bruno Ngenze.

Daktari Bruno Ngenze, Mkuu wa Shirika la afya dunianni, katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri alipozungumza na mwandishi wetu Tschube Ngorombi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.